Vioja vya watoto wadogo (0-5years), tuambie vioja vya mwanao

Vioja vya watoto wadogo (0-5years), tuambie vioja vya mwanao

Mtoto anam-miss mama ila haya majibu yenu yananishangaza mpaka basi. Kwa hiyo wewe huleti mke mwingine kwa sababu mke wako atalia? If he is real your friend, make the best of it. Teach him principles. Mtoto akikuuliza kitu mwambie ukweli wa hicho kitu hata kama si ukweli wako. Akihoji ukweli wako ndo ujieleze.
Thanks ....i will make the best of it!wasalim airtel
 
Watoto wanafundishika. Ukimkanya kitu kwa karipio, hatathubutu kukirudia. Tabia ya kulea watoto kama mayai ndiyo inayo waharibu.

Hata kukaripia kunaharibu watoto. Watoto wote wenye akili timamu wanaokulia kwenye mazingira ya "literacy" wakifikia umri fulani huanza kushika kalamu na kupenda kuchorachora huku wameshika kalamu kaa vile mkuki. Wakianza shule ile hali ya kuandika andika huzidi na kutokana na ufahamu mdogo na shauku kubwa huandika popote. Kazi ya mzazi si kukaripia bali kutoa mwongozo kuwa achore chore na kuandikia wapi na si kumkaripia.
 
Miye wangu anapenda kufuatilia naongea na nani, utamsikia 'nani" namjibu rafiki yangu, atauliza tena anasemaje??? Nilichogundua yupo katika umri wa kuhoji, she is 2.4. Yaani kuna wakati nawaza sijui katumwa na mama yake anifuatilie nazungumza na nani!!!
Na tangazo la airtel kuna vikatuni vinaobesha vidole viwili analipenda hatari.
 
Karibu na tunapoishi kuna lodge ya kitalii, mtoto wangu wa miaka sita na wenzake walinyimwa kuingia akamwambia mlinzi "mbona tukija na mummy hautunyimi kwanza mama yangu amesema ananunua hii hotel". Yule mlinzi mbona aliwaruhusu. Baadaye mlinzi alikuja kuniuliza kama ni kweli hotel ilikuwa inauzwa. Nikiwa nashangaa kwa nini ananiuliza mimi, akaniambia 'mtoto wako kasema unainunua'. Mlinzi was so worried. Niliposikia story yote kutoka kwa dada nilimuelwa yule mlinzi.
 
Wangu ana miezi 9.5 anaita Baba,Mama , muda mwingi ana nisemesha mambo ambayo mimi siyaelewi yani eeeeb dadasa dodoo me huwa nina mwambia sawa kabisa anafurahi au wakati mwingine ninamwambia adi kesho anongea wee me nina mwambia swa kabisa!!! nifanye nini sasa wakati lugha gongana hapo!!
Au wakati mwingine nina mwambia mwambie mama yako
 
Halafu wangu haniiti baba, yeye ni mwendo wa kuniita baba Grace, vile anavyoniita mama yake.
Wakati wa kulala, nikimuambia sali, anagonga ile sala ya kuombea chakula, nadhani RCs wenzangu wanaipata hiyo.
 
Kuna watoto wengine wanachagua watu..akiwa analia ukitokea wewe ananyamaza na anakukimbilia umbebe!!
inategemea, ni lazima utakuwa umevaa fresh pia una mawe mfukoni ama kwa pochi na mkononi una smartphone iphone 7 plus la nguvu!!. This is natural bila maelezo ya ziada.
 
Miye wangu anapenda kufuatilia naongea na nani, utamsikia 'nani" namjibu rafiki yangu, atauliza tena anasemaje??? Nilichogundua yupo katika umri wa kuhoji, she is 2.4. Yaani kuna wakati nawaza sijui katumwa na mama yake anifuatilie nazungumza na nani!!!
Na tangazo la airtel kuna vikatuni vinaobesha vidole viwili analipenda hatari.
Huyo mtoto ni mdadisi sana. Hilo hayo maswali ya "nani" na "anasemaje" yanafurahisha sana.
 
Siku ya Jumamosi alfajir mwanangu 5yrs aliamka saa kumi na moja. Akasema wanamitihani ya kufunga nusu mwaka.
Mke wangu akamuomba alale kidogo kwamba muda bado. Akaamka around saa mbili kasoro. Akagundua ilikuwa weekend

Jumatatu akaingia darasani kama kawa ile narudi jion nakuta taarifa alirudishwa ada sh 20000/ Roho iliniuma sana malaika huyu. kutoka Mil 1.2 kwa mwaka 20 elfu unamfukuza mtoto?

Kwa sasa namuhamishia shule nyingine
Dah inauma sana, hawajui jinsi gani mtoto alivyokuwa na juhudi. Hakustahili kuadhibiwa yeye.
 
inategemea, ni lazima utakuwa umevaa fresh pia una mawe mfukoni ama kwa pochi na mkononi una smartphone la nguvu!!. This is natural bila maelezo ya ziada.
mmmmh wewe sidhani kama tupo pamoja
 
Huyu dogo an 3Yrs

#1. Siku moja aliniambia "Baba nataka kuolewa"... Nikamuuliza unataka kuolewa na nani akanijibu " na wewe"..... Nikapigwa na butwaa.


#2. Siku nyingine akaniambia "Baba nina mimba".... Nikajifanya kama sijamsikia.


#3. Siku nyingine akaja na ua anaiambia "Baba ua la bibi harusi".

#4. Siku moja nilienda naye nyumbani akamuuliza baba yangu " Babu wazazi wako wapi?.... Baba akamjibu " wamefariki"... Dogo akasema "unaishi vipi bila ya wazazi".


Hayo ni machache
Mtoto wako anatazama movie kama za bongo movie ndio maana amejua kuna kitu kinaitwa mimba na kuolewa au amejifunza kutoka kwa watu. Katika umri huo ni mapema mno kufikiria mambo hayo.
 
Back
Top Bottom