Vioja vya watoto wadogo (0-5years), tuambie vioja vya mwanao

Vioja vya watoto wadogo (0-5years), tuambie vioja vya mwanao

Huyu dogo an 3Yrs

#1. Siku moja aliniambia "Baba nataka kuolewa"... Nikamuuliza unataka kuolewa na nani akanijibu " na wewe"..... Nikapigwa na butwaa.


#2. Siku nyingine akaniambia "Baba nina mimba".... Nikajifanya kama sijamsikia.


#3. Siku nyingine akaja na ua anaiambia "Baba ua la bibi harusi".

#4. Siku moja nilienda naye nyumbani akamuuliza baba yangu " Babu wazazi wako wapi?.... Baba akamjibu " wamefariki"... Dogo akasema "unaishi vipi bila ya wazazi".


Hayo ni machache
 
Mimi mwanangu ana miaka mitatu aliniuliza mbona mama nikimwita Asha (sio jina lake halisi) ananichapa lakini wewe mbona hakuchapi?
Mwambie Asha asimchape mtoto mdogo kwa kitu kidogo namna hiyo. Atamchanganya na kumjengea chuki bila sababu ya msingi. Hakuna ubaya mtoto kumwita mama yake Asha. Akitaka amwite mama Bakari basi wewe mwite hivyo na nyumba nzima imwite hivyo ili awe na "input" moja tu ya jina la mama mnalotaka alitumie. Nilishaona mtoto mkubwa tu kapotea kapelekwa ITV anaulizwa baba/mama anaitwa nani hajui anasema "anaitwa mama" au "baba". Mtoto wangu akiwa na miaka miwili na nusu alikuwa anajua majina yangu yote matatu na namba zangu za simu na kazi yangu. Wakati akikua alikuwa akisikia nikiitwa Nandera, nikiitwa dada na yeye alikuwa akiambiwa nenda kwa mama, mpe mama ..... na kadri akili yake ilivyokuwa ikikua naye alikuwa akiongezeka uwezo wa kuelewa na kutofautisha mambo kulingana na muktadha. Mtoto wangu sasa ana miaka 9, ni rafiki yangu sana na kuna wakati huniita jina langu la kwanza, lakini huniita tukiwa wawili tu maana anajua akiniita mbele za watu huku uswahilini atatafsiriwa hana heshima. Nilimwambia asiniite Nandera tukiwa kwenye mazingira fulani nilipoona anaweza kuelewa sababu. Nyie kama mnaona mtoto akimwita mama yake jina la kwanza si adabu basi tafuta njia nyingine ila si kumchapa. Mnaweza tu kumwambia mama anaitwa Asha na watu wazima tu mkaishia hapo.
 
Jembe langu lina miaka3,akimuona mtu flani akiongea kwenye tv,anakimbilia remote na kubadili chanel.Simply ana aleji naye.
Huyo mjukuu wangu atakuwa hapendi hata baadhi ya rangi hasa za mimea. Mweke mbali na viberiti asije akachoma misitu.
 
Kwa hiyo u
Mwanangu (5): Baba mbona unapunguza mwendo??
Mimi: Kuna askari mbele
Mwanangu: Sasa usipopunguza mwendo atakufanyaje?
Mimi: Atanikamata
Mwanangu: Atakukamata atakufanyaje?
Mimi: Atanifunga kamba anipeleke gerezani kunifunga.
Mwanangu: Police kazi yake kufunga kamba watu?
Mimi: Ndiyo, ila wale wakorofi tu.
Mwanangu: Hata watoto wadogo anawakamata na kuwafunga?
Mimi: Ndiyo, lakini wale watoto wakorofi wasiopenda kufanya H/W
Mwanangu: Mimi si mkorofi na nafanya HW, si ndiyo baba
Mimi: eeeee
(Tunawakaribia Police wa usalama barabarani tunawapita)
Mwanangu: Police nimewaona watatu pia kuna Mwanamke, baba hata Police Mwanamke yupo
Mimi: Ndiyo
Mwanangu: Na yeye anaweza kukamata watu na kuwafunga?
Mimi: Ndiyo:
(Ukimya dakika 2)

Mwanangu: Baba weka speed One hundred tumeshawapita ma police. (huku akiangalia mshale wa speed-meter)

-------------
Kwa hiyo unamwambia afanye makosa ilimradi asikamatwe; asifanye mambo sahihi kwa sababu ni sahihi bali kwa sababu hakuna mtu anayemuona; polisi wanaweza kudanganywa, hivyo hata baba, mama, mwalimu.... naweza kuwafanyia ujanja wasijue makosa yangu. Rekebisha mkuu. Tunapunguza mwendo kwa sababu ya usalama, na mwendokasi ni hatari.
 
Mwanangu 3 years, juzi aliniita akaniambia baba, kunguru anamchukua karanga, nikawasimuelewi nikamwambia twende nje ukanionyeshe.
Kufikanje akanyooshea kidole kifaranga cha kuku akasematena, namnukuu, "anamchukua kungulu kalangahuyuapa" hukuanamnyooshea kidole kifaranga cha kuku daah, nilichekasana, jinsi anavyo muita kifaranga eti, karanga.
 
Mmenikumbusha kuna siku mwanangu(5yrs) alinichekesha sana.Nlikua jikoni napika half cake akaingia akaniuliza "mama ivi jana nlikusalimia"nkamjibu hapana( makusudi nijue lengo lake),akaniambia "nkusalimie sasa hivi?" na mimi ee.Alivomaliza tu kunisalimia "mama naomba half cake "
 
Mi mwanangu kuna siku nimetoka kazini nimechoka, mama yake yupo mbali kikazi...akaniambia baba kwanini usiwe na mke mwingine, yani alikua very serious!!!nikamwambia mama yako akijua atalia sana, akanijibu mama akiwa anakuja unamwambie mwingine aondoke mpaka mama atakapoondoka......aisee ni mengi sana, ila kwa kifupi he is real my friend.

Mtoto anam-miss mama ila haya majibu yenu yananishangaza mpaka basi. Kwa hiyo wewe huleti mke mwingine kwa sababu mke wako atalia? If he is real your friend, make the best of it. Teach him principles. Mtoto akikuuliza kitu mwambie ukweli wa hicho kitu hata kama si ukweli wako. Akihoji ukweli wako ndo ujieleze.
 
Back
Top Bottom