Nilipomaliza chuo nilifanya kazi kampuni moja ya binafsi, ilikuwa ya ukandarasi huyo bosi alikuwa na watoto 6, kati ya hao mmoja tu ndio alikuwa wa kiume na wa mwisho mwisho kuzaliwa, akawa anasema natamani ingekuwa na uwezo wa kumvuta mtoto akue haraka ili huyu jembe anisaidie majukumu wakati huo alikuwa class seven, sasa hivi yule kijana kamaliza chuo ana degree baada ya kumaliza form four pale ST.. Costantene Arusha akampeleka chuo Nairobi, ila jamaa amekuwa MZIGO, ZOBA yaani hana afanyalo pale zaidi ya kuendesha magari ya baba, siku moja nikaenda kusalimia maana nilishaondoka kitambo hapo, nikamuuliza vipi sasa amekua kuna msaada unaopta kama ulivotamani kumkuza fasta, aliniangalia kwa huruma sana yaani kama anajuta mtoto kukua, alijua acha tu nibebe msalaba wangu nikifa vikiisha basi sitakuwa na la kulaumiwa, nilimuhurumia.. Alipokuwa mdogo alikuwa anapenda sana kuja ofisini na hukaa na mzee wake kwa umakini kama kuna jambo ana hakikisha haliharibiki.