Vioja vya watoto wadogo (0-5years), tuambie vioja vya mwanao

[emoji23] [emoji23] [emoji23] Lol, huyu bingwa kiboko hafai duuh, nimecheka sana
 
Wa kwangu kipindi ana miaka miwili mpaka mitatu aje chumbani kwetu akute mmefunga mlango balaa lake mpaka majirani watajua, hivyo kama mlango umerudishiwa akiugusa tu lazima mmoja akimbie kuufungua kabla ya hajaanzisha timbwili
 
Huyu atakuwa ana elements za amphibia....[emoji2]
 
Nimewakuta watoto mtaani nikawapa chemsha bongo kuwa kwenye pipi tano ukitoa pipi moja zitabakia pipi ngapi?

Walichonijibu sasa[emoji23]

Eti tuonyeshe kwanza hizo pipi[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
leo nimenunua maparachichi ile kuingia ndani tu yeye kayapanga kayapiga kama mpira,nimetoka maparachichi yamekua rojooo...mwenyewe anaita mama mpiraa goooo....
[emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Wako wawili mdogo around 5 years. Tulienda bookshop na wote wawili, huyu mdogo yeye kitabu kikiwa size ndogo akajua ni chawatoto. Akajikusanyia vitabu kadhaa vyenye size ndogo akaleta kwa cashier. .
 
Mi mwanangu akisikia simu inaita hata kama alikuwa anacheza atakimbia kuniletea,anafurahi sana akiona naongea na simu ana mwaka na nusu bado hajajua kuongea anajua haloo na neno poa.
Hahahaaaa...Kama wangu hapa!!
 
Hapa nadhani hawa wanao wakalelewe jirani na mahakama
Na ikiwezekana wakae karibu na TL manake si kwa ukatili huu
 
Hapa nadhani hawa wanao wakalelewe jirani na mahakama
Na ikiwezekana wakae karibu na TL manake si kwa ukatili huu
 
Dogo ana miaka(4.6)akigundua kuwa umedanganya,utackia anasema ACHA MANENO YAKO BWANAA huwa naenjy sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…