Aisee mie sitaki hata kukumbuka,mwanang alikuwa mtundu balaa at least sasa hivi nimepumua,wakati akiwa na miaka mitano akiwa shuleni (boarding) sijui alitoa wapi mfuko ule wa Salfeti akawachukua watoto wadogo watatu akawafungia kwenye mfuko halaf akawaambia atakayepiga kelele namchapa viboko,akatoka akaenda kucheka bahati nzuri mwalimu akapita pale akaona mfuko unacheza cheza akashangaa kuufungua akakuta watoto walishaanza kuchoka, huku na huku nani kafanya hivi wakamtaja,mwalimu wake ananipigia simu mwanao leo kafanya kosa hili yaani nliishiwa pozi, nkaenda shuleni kwao namuuliza akanambia ahaa niliwaweka watulie maana walikuwa wanasumbua,siku nyingine karudi likizo niko kazini , akaweka Cd tano kwenye radio inayobeba cd tatu, nilivyorudi kanipokea getini akanambia yaani Mom radio yako imegoma kabisaa kuimba leo ahaa itakuwa ulinunua radio ya kichina,nafungua pale kaweka cd kushinda uwezo na sijui alichokonoa nn radio ikafa kabisaaaa