Vioja vya watoto wadogo (0-5years), tuambie vioja vya mwanao

Atakuja kuwa Iddi Amini huyo.
 
Mie nimeipaka juzi juzi tu hapo. Nayo ishachorwa zamani. Patterns na days na dates.
Suluhisho ni kupaka rangi washable. Silk au water guard. Wakichora unaweza kufuta.

Bora umenipa akili mumy
 
namba 3 hiyo....simu ya wyf daaa[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
mi wangu miaka 3 now....nilimnunulia baiskeri tulilala saa nane usiku siku hiyo....anaendesha chumbani....mbaya zaid anataka muwe wote...akikwama umsaidie kumgeuza#nakupendamwanangu#
 
Wangu sijui angekuaje, ametangulia mbele ya haki, katakua mbinguni kanacheza huko...
Pole sana Mungu aendelee kukufariji. Naamini yeye aliyekupa na kumchukua huyo was kwanza, atakupa faraja nyingine. Amini mwanao ameungana na malaika na anafurahinna kukuombea huko alipo.
 
Kama ni nyumba ya kupanga andika maumivu zaidi maana mwenye nyumba akijua ni hatari sana.

Kweli mkuu, yaan hapa kabla sijahama nitahakikisha naipaka rangi. Hapo ni intro sasa kila nikirudi home panaongezeka...

Tatizo huwa hawakubali kuandika eneo moja, let say unampa ubao ataandika ubaoni baadae atasahau atarudi mule mule
 
Kubwa kuliko alikua anacheza na wenzake wakamtania "mwangalie kichwa chake" duuh karudi amekasirika analia anasema "baba hiki kichwa sikitaki niletee kingine" Ilibidi niuvae ubaba kumtuliza.
hahahahahahahaha
 
mtoto wa rafiki yangu 4yrs mda wote yeye ni kuangalia katuni ila akimuona mama yake tu anabadilisha station anaweka sinema zetu ili apate chance ya kucheza game kwenye simu ya mama ake
 
[emoji23][emoji23]
mimi nmelea watoto wengi.
jamani huyu mmoja alikua ananiimbia Dar mpaka moro, Anakwambia "Wapi Dar mpaka Bo.ro" [emoji23]
akila anakwambia baba unato
mba mboga (unakomba mboga) mama anaondeza tu(anaongeza)[emoji23][emoji23]

sasa hivi yuko secondary mbaba, mwingine yuko Darasa la 5 mdada
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…