Vioja vya watoto wadogo (0-5years), tuambie vioja vya mwanao

Wa kwangu Mwaka 1.7 hampendi Kunguru akimuona tu lazima amponde kwa mawe, Akilala usiku alafu Mvua akiwa inanyesha anaanza kulia "Mama Kunguru anakuja, Baba Kunguru anakuja" basi atalia weee mpaka Mvua iishe ndio analala! Najiuliza Hivi Kunguru alimfanya nini?mpaka leo sijapata jibu!

Alikuwa hafahamu kutamka vizuri neno Kikombe alikuwa anatamka "Kitombe"

Hapendi Ugali, Ukipika Ugali unaula mwenyewe. Yeye mpe wali hata kama ni kidogo kwake ni sawa tu!
 
mie wangu ana 6months,yeye tangazo likitokea lazima ainuke kichwa kulitazama,awe amelala lazima ataamka,likiisha tu anaendelea kulala.
 
Mtoto wa mama mwenye nyumba anampenda sana demu wangu akija lazima na chenyewe kitie timu.. kinanikoseshaga na kunicheleweshea mzigo
 
Wangu 2 years Jana anaangalia juu akaniambia (Baba nani anafua kule juu ona mapovu ni mengi)
Note: mapovu-mawingu
 
Umesahau, kituko Kingine cha kupenda kuvaa ndala mpindule
 

hahahaha jamani eti na ww atakuwa anakupenda sana babaake... they are so innocent yaani
 
Wangu ni 3yrs now amewah kuniuliza nilimtoa wapi nkamdanganya nilimnunua dukan akakaa kimya kama dk 3 akanirushia swali tena "sasa baba mbuzi anapata wapi hela ya kununua mtoto".nlijikausha kama vle cjamsikia bahat nzur mama yake akamwita akanywe maziwa
 
Were mtoto nani kakhukwaruza hapa karibu na jicho?
Sijui.
Wangekutoboa jicho!
Shindwa baba sitoboki jicho. (5 yrs)
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
Uongo una kikomo mkuu
 
Mwanangu 2.5 anapenda kujiremba akimuona mama yake kapaka poda mwenzangu anatafuta ngano ilipo
 
Niko ughaibuni ana miezi 4 hajaniona ila hata alie vipi nikipiga sim nikiita baaba ananyama kama anaelewa vile
 
wa kwangu ana 3 yrs kila kitu kizuri kanunua baba yake yaani hata ukiwa unamlisha ukisema chakula kizuri atakwambia baba yake kapika yeye na babake hadi raha sijui ndio ule msemo mtoto wa kike na baba na wakiume na mama.
 
mtoto wa shemeji yangu miak 2 ni balaaa
anapenda niita dogo badal ya ba mdogo
Ukimkuta katoka kuoga tuu anajificha papuchi anakusemea mama dogo ananchungulia au utasikia mama kaka anamchungulia dada ake
ana vituko balaa kuna kitoto cha jiran anakipenda balaa anakiita mchumba kula lazm amtafte kuoga pia lazm
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…