Vioja vya watoto wadogo (0-5years), tuambie vioja vya mwanao

Jembe langu lina miaka3,akimuona mtu flani akiongea kwenye tv,anakimbilia remote na kubadili chanel.Simply ana aleji naye.
Mi la kwangu lina miaka 30. Juzi limeniletea binti wa 6 mwenye ujauzito wake. Mzee mzima nakaribia kupata mjukuu wa sita toka kwa mabinti sita tofauti.
 
Jembe langu lina miaka3,akimuona mtu flani akiongea kwenye tv,anakimbilia remote na kubadili chanel.Simply ana aleji naye.
Tatizo jiwe anatisha na ile solar panel mmmh!!!!
 
Dah!! Poleni kwa visa vya watoto wenu.
Ila naamini na nyinyi mliwafanyia visa wazee wenu kwa hiyo tulieni.
 
Mi la kwangu lina miaka 30. Juzi limeniletea binti wa 6 mwenye ujauzito wake. Mzee mzima nakaribia kupata mjukuu wa sita toka kwa mabinti sita tofauti.
Hongera umekuza/lea!
 
Uzi bora kabisa Huu. Unahamasisha malezi yenye upendo kwa familia.
 
Jf kiboko. Kikombe anasemaa ???
 
wale tusio na watoto hebu tubane kwa pembeni hapa kuona wenzetu wanavyo-enjoy maisha kufurahi na watoto
 
Watoto wana mambo mengi sana ya hatari na ya kuchekesha pia.

Penda sana jembe langu, alinikuta naangalia concert ya Peter Tosh akatulia tulii akawa makini kweli kuangalia sasa kazi ikaja siku nataka kumnyoa nywele asee dogo akaanza kukataa kunyolewa nywele eti ananiambia 'babaa kulee' ase nlipogundua anamuongelea Peter Tosh nlimcheka sana nikaona nimuache nazo adi siku zimkere ndio nimnyoe. Leo zina kama miaka 2 hiv hana mpango wa kuzichukia kabisa.

Ni ka dreadboy sijui shule itakuwaje mwakani. Hadi namsikitikia anavyopenda nywele zake. Utafikiri ni kamtu kazima vle.
 
Dogo 2yrs anapenda magari jana kaona vikatuni vinachezea magari akasogea kwenye tv akaanza kusema aomba gaii huku ananyosha mkono
 
Wa kwangu akiniona tu hata kama alikuwa anacheza basi ataangua kilio sijui kumchongea dada wa kazi kampiga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…