Vioja vya watoto wadogo (0-5years), tuambie vioja vya mwanao

Hongera kwa kuzaa Mkorea
 
Bila picha za watoto hapa mimi siwalelewi chochote
 
Ngoja nilete vyangu kidogo kutokea ofisini....

Mimi ni mtu ambaye inapotokea nahudumia mtoto mara nyingi najitahidi kuwa nao karibu sana ili wasiiogope huduma hata inapotokea umemuandikia sindano....

Basi, kalikuja katoto kasichana umri 3 hivi sasa alikuja na mama yake kwenye huduma... Huku mama yake ndiye Mgonjwa wakati huo... Wakati matibabu yakiendelea huku nikimuhoji Mama yake, aliniuliza... Wewe Uncle unaitwa nani? Nikamwambia naitwa Baraka basi akaridhika akatoka nje.... Nikaendelea na kumuhudumia Mama yake nikamaliza nika oder akafanye vipimo, alipoondoka Mimi nikatoka nikaenda dukani...

Niliporudi Mama yake akaniambia, Mtoto wake kaniulizia kuwa Baraka yuko wapi [emoji23][emoji23][emoji23] nilifurahi mnoo kusikia hivyo...

Baada ya huduma kuisha nikampa mtoto zawad ya notebook na peni mpya akasema asante akaondoka na mama yake....

Zilipita kama siku nne hivi, mchana wakati naenda nyumbani nikaona watoto wanatoka shule wanaenda majumbani mwao... Wakati nawashangaa kwasababu huwa napenda kuwatizama wakiwa wanacheza cheza na uniform zao ... Ghafla nikaona katoto kanakuja mbele yangu kanalia, nikakumbuka ni yule niliyempa zawad basi kakaniita Baraka huku analia, nikachuchumaa kanihug halafu akasema Baraka yule Mtoto amenipiga, nikawaita wote nikawafundisha wasipigane....

Kisha nikamfuta machozi akaridhika nikamuaga akaenda na wenzie kwao huko...

Nilijihisi furaha sana sana kwasababu sina mtoto hivyo nilijiona nimepewa heshima kubwa kwenye kizazi kijacho....

Nilichojifunza, watoto ni Baraka na furaha yako kwao huacha alama isiyofutika maishani mwao....
 
Oooh waoooh
 
Safi Doc
 
Subiri afikishe 15 yrs, utakuja kutupa mrejesho!
 
Jiandae kumla mama yake kimasihara
 
Wa kwetu ana miaka 1.5 na hajaweza kuongea bado...

Vituko vyake ni vingi ila kikubwa ni kwamba anaamka asubuhi sana na ukimvalisha tu breki kwa majirani kuwagongea...

Toto kwake ni mtoto, ya moto na moto lakini kuna watu akiwaona anawaita toto, toto...

Tutu kwake ni dudu au jina lake akimaanisha Fatuma maana kuna wanaomwitaga jina hilo kwa kila namna mtu anavyojisikia. Basi nae kuna watu akiwaona anawaita tutuu...

Hapa nyumbani kuna paka ambaye wanacheza wote aisee hata mtoto awe analia vipi au anashughuli gani wewe fanya "nyau" lazima atanyamaza ili akazie na yeye "nyau". Kuna watu akiwaona anawaita nyau (mpaka mimi baba yake naitwa/tunaitana nyau)
 
Mie huwa nafurahishwa na tabia ya wtt kukimbiakimbia. Yaani we Mtume chumbani from sitting room. Izo mbio zake yaani hakuna kutembea. Ivi ni kwa nini? [emoji1787]
Umenikumbusha nilivokua dogo mama akiniagiza nikaangalie ndani ni saa ngapi zile saa za ukutani, basi natoka mbioo😂😂 hadi naambiwa nenda taratibu utaanguka wewee😂
 
Umenikumbusha nilivokua dogo mama akiniagiza nikaangalie ndani ni saa ngapi zile saa za ukutani, basi natoka mbioo[emoji23][emoji23] hadi naambiwa nenda taratibu utaanguka wewee[emoji23]
Na wanaanguka kweli. Utakuta mtu huku mkononi kabeba kitu lkn mabioo. Ataanguka, atalia utamwambia Pole, lkn akiinuka hapo mbioo nyengine keshasahau zamani km katoka kuanguka.

Mie huwaambia miguu mtaitia makovu ya vidonda hlf mkiwa wakubwa mjichukie [emoji23]
 
[emoji28][emoji28] huyu wangu (7 years) hapebdi kuagizwa ….. yaaan ukimuagiza dukani mnakosana yeye n TV, TV na yeye kazi kwelikweli
serious!? Na wewe una mchekea tu!?
Aya bhana ngoja nisiingilie malezi yako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…