Vioja vya watoto wadogo (0-5years), tuambie vioja vya mwanao

Vioja vya watoto wadogo (0-5years), tuambie vioja vya mwanao

kuna haka kamoja ndo balaa kabisa,
mama: itabdidi uhame chumba umeshakuwa mkubwa, kitanda hakitutoshi watatu!!
mtoto: kwani mi na baba nani mkubwa?
mama: baba......
mtoto: basi baba ndo ahame yeye ndo mkubwa kuliko mimi!!!!!!
mama alikosa jibu. watoto burudani sana aisee, mnaweza mkawa mnacheza naye anacheka lakini ndani ya dakika moja akaaza kulia unashindwa kuelewa imekuwaje.
Maswali yaliyoenda shule![emoji23]
 
wa kwangu miaka 3 kila shughuli ya nyumbani anataka aifanye apike yeye,aoshe vyombo yeye afagie yeye ili muradi asikuone unacho kifanya anatamani afanye hivyo sasa huko shule ndo balaaa akirudi anaigiza kila walimu walichokifanya au kuongea! NI RAHA KWAKWELI!
 
wanaume wana wivu sana,, naanza kugundua watoto wakiume wanawivu sana natural,,, hope una enjoy kulea mkuu!! Huoni kero
Naenjoy sana, sipati picha huko mtaani lione wababa wanamuongelesha mama yake.... Litakua linanuna sana hili toto langu
 
Mada kama hii huwa zinaletwa na wanawake halafu wanaume ndio wanachangia.

Sasa kidume mzima unajipinda unaanzisha uzi kama huu....!!!!

Unatukosea sana wanaume wenzako.
Wanaume mnaojihusisha na mambo ya jinsia moja huwa mnajishtukia sana, sasa mwanaume rijali uliezalisha ukijisifia kuhusu mtoto wako nao sio uanaume? Haya tukupishe ww umsifie bwana wako
 
Jembe langu lina miaka3,akimuona mtu flani akiongea kwenye tv,anakimbilia remote na kubadili chanel.Simply ana aleji naye.

hahhhaha nimecheka aic huyo yuko km wangu akimuona yule wa upande wetu hureeeeee anaita kbs mamamaaaaaa LOWASAAAAAAAAA
 
Watoto raha JAMANI wakwangu Ana 1.5 yrs ananishangaza yeye hana shida na simu ubaya isahau kwenye Kochi alafu iite, niatakuja speed huyo kama faru ataichukua nakuipigiza chini mpaka ife then anaendelea nashuguli zake.
 
Aisee mie sitaki hata kukumbuka,mwanang alikuwa mtundu balaa at least sasa hivi nimepumua,wakati akiwa na miaka mitano akiwa shuleni (boarding) sijui alitoa wapi mfuko ule wa Salfeti akawachukua watoto wadogo watatu akawafungia kwenye mfuko halaf akawaambia atakayepiga kelele namchapa viboko,akatoka akaenda kucheka bahati nzuri mwalimu akapita pale akaona mfuko unacheza cheza akashangaa kuufungua akakuta watoto walishaanza kuchoka, huku na huku nani kafanya hivi wakamtaja,mwalimu wake ananipigia simu mwanao leo kafanya kosa hili yaani nliishiwa pozi, nkaenda shuleni kwao namuuliza akanambia ahaa niliwaweka watulie maana walikuwa wanasumbua,siku nyingine karudi likizo niko kazini , akaweka Cd tano kwenye radio inayobeba cd tatu, nilivyorudi kanipokea getini akanambia yaani Mom radio yako imegoma kabisaa kuimba leo ahaa itakuwa ulinunua radio ya kichina,nafungua pale kaweka cd kushinda uwezo na sijui alichokonoa nn radio ikafa kabisaaaa
Dogo mDaDisi sana huyu, NimempenDa buree kabisaa
 
Sikubali hakyanani sikubali namfata mwanangu , mama mkwe ntakulipa tu mahari yako nirudishie mke wang na mwanang , ona sasa mi nitaeleza nini hapa' mke wang toka amejifungua huu mwezi wa pili umeisha bado unawang'ang'ania tu aaaaagrahhh!!!???
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
anDika tu mkuu
 
Hili toto langu la kiume la mwaka mmoja halipend niwe karib sana na mama yake, hata tukikumbatiana tu mbele yake linaanza kulia, kituko chake kikubwa mkianza kugegedana ni lazima lishtuke na linaanza kunitoa nisiwe juu ya mama yake
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
bint yangu ana miaka 3 kila siku analia nimpeleke Kolomije... nikimkatalia ananiita 'Bashite wewe'
 
mpaka kufikia page hii ya tatu, inaonekana watoto wengi wa siku hizi wanapenda sana simu, naendelea kusoma.
Same thing I Was thinking
halafu ambao wana akili za kuDadisi pia ni Wengi..
WasiopenDa mama zao wasiguswe wamo pia kiaina
 
Mi wangu mapacha, wana miaka 3.5, kila nikirudi home lazima wanikimbilie na kunikumbatia sasa siku wakichelewa wakakuta mama yao kaniwahi nimemkumbatia wanaona aibu wanarudi ndani mbio,
Kipindi wakiwa na mwaka na nusu mmoja wao ilkua ukimkera akikasirika anajirusha rusha hasa akiwa kitandani au kwenye kochi, siku moja kajichanganya kajirusha kwenye tiles alivyoumia hakurudia tena!
Siku nilimtuma rafiki yangu aende kuchukua gari home walilia sana huku wakisema "gari ya baba, gari ya baba" ilibidi nipigiwe simu niongee nao ndo wakaacha kulia nda jamaa akaondoka na gari.
Huyu mdogo ndo anapenda kuchezea simu ya mama yake balaa ukimnyang'anya analia sana, ila yangu ukimnyang'anya halii!
 
Back
Top Bottom