Vioja vya watoto wadogo (0-5years), tuambie vioja vya mwanao

Vioja vya watoto wadogo (0-5years), tuambie vioja vya mwanao

[emoji23][emoji23]
mimi nmelea watoto wengi.
jamani huyu mmoja alikua ananiimbia Dar mpaka moro, Anakwambia "Wapi Dar mpaka Bo.ro" [emoji23]
akila anakwambia baba unato
mba mboga (unakomba mboga) mama anaondeza tu(anaongeza)[emoji23][emoji23]

sasa hivi yuko secondary mbaba, mwingine yuko Darasa la 5 mdada
[emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Wangu ana 4yrs last week walikuwa kwenye exam ya midterm kwa elimu yake ya kindergarten sasa mwalimu akaandika vitu amabvyo hawajawahi kusoma aisee aligoma kuufanya huo mtihani mpaka akaenda mama yake siku iliyofuata ikabidi afanye kama special mbele ya mama yake na kumbembeleza kwa sana tu.
Hako University kataongoza migomo sana.
 
Wa kwangu amewahi niambia hampendi mzee Mag... Ana sura ngumu baada ya kumuona TBc
 
Wa kwangu atatimiza 4yrs next month. Ananipenda sana na mm nampenda sana.
Utundu umepitiliza. Kuta zote zimechafuliwa kwa kuchorwa ni hatari.
 
Wangu alichukua mtihani kuja kufanya nyumbani dada amsahishie mbona kila Siku huwa anamsahishia zoezi basi na mtihani asahishe.
Doto anamwambia baba sisi wanaume au wanawake kama mama?baba akajibu wanaume anamwambia sasa si uje ulale huku chumbani kwa wanaume mbona unalala chumbani kwa wanawake!
 
Watoto wana vioja na story nyingi sn na huo ni wkt mzuri sn wa kumsoma mtoto wako na kuchukua hatua za kumsaidia
 
Nilivyoona hii picha nikakumbuka vituko vya humu[emoji23][emoji23][emoji23]
 

Attachments

  • 1497613262602.jpg
    1497613262602.jpg
    74.3 KB · Views: 74
Jembe langu lina miaka3,akimuona mtu flani akiongea kwenye tv,anakimbilia remote na kubadili chanel.Simply ana aleji naye.
Sijajua ila naisi ni naniliuuu ana aleji nae[emoji12] [emoji12] [emoji12] [emoji12] [emoji12]
 
Wangu alichukua mtihani kuja kufanya nyumbani dada amsahishie mbona kila Siku huwa anamsahishia zoezi basi na mtihani asahishe.
Doto anamwambia baba sisi wanaume au wanawake kama mama?baba akajibu wanaume anamwambia sasa si uje ulale huku chumbani kwa wanaume mbona unalala chumbani kwa wanawake!
Baba analala Na wanawake Sio? Dogo jiniaz
 
Wa kwangu akiwa na 3yrs nilikuwa nampeleka sehemu akabembee, tukiwa njian kuna jamaa akanipigia simu tukaongea, katika maelezo yangu sijui aliniuliza nini nkamwambia nipo njian nampeleka dogo sehemu akachezecheze, baadae yamepita masaa kama manne hivi tukiwa njian tunarudi akaniukiza swali, eti baba kwani mimi naitwa nani? Nkamwambia Joyce, akaniuliza sasa mbona mda ule uliniita dogo? Hahahha, loh, nilikuwa mpole kama piriton
 
Hahahaaa, huyu mdogo wa kike ndiyo huwa ananikata maini, yaani keshanifanya mtumwa kabsaaa mpaka mama yake analalamika kwamba nampendelea! Kana mitego hakooo, na kanamacho ya kubembeleza hakooo...hata ukitaka kukatandika utashuka mwenyewe, sijuwi ndiyo watoto wa kike wote wameumbwa hivyo! 4yo na kako smart vibaya darasani, ila sasa nina mashaka nako sana kakikua itakuwaje, maana kanapenda sana simu, simu iwe ya tochi au smartphone atatafuta game lolote huyu mtoto na atalicheza utashangaa anapata score za ajabu wakati mimi siwezi hata kulicheza, kanapenda simu balaa......haka kakihongwa simu kweli katakataa?!...hapa dawa ni kukapatia kila kanachotaka.
Usiwaze vibaya my dearmuombee mtoto,mtoto wa like haina kubwa,hawezi kukuuza hata iweje,wanazaliwa namfupa kwenye nguvu ya uchungu wa uzazi
 
Wangu ni wa miezi 3 sasa , kanapenda starehe sana, anapenda abebwe na uwe unafanya safari. Akishiba anapenda sana kucheka, njaa ikimuuma hana urafiki na mtu ni mwendo wa kulia. Anapenda kutazama video au kukaa nje aone mwanga.
 
Kuna katoto kana miaka 9 now haongei kwa ajili jiyo nadhani na uoga wa wazazi kutomkata umechangia, na ile imani kwamba akifika miezi 6 kama hajakatwa haongei tena kumbe ni uongo tu wa mitaani.

Na wengine uzembe unachangia mtoto akizaliwa inabidi uchunguze kiungo kimoja baada ya kingine ili kama ni tatizo lishughulikiwe mapema. Mtoto wenye 'Udata' akiwa analia utagundua tu uliaji wake haupo sawa
Mimi wangu nilimkata mwenyewe na kiwembe akiwa na siku 40
 
Nina watatu hao hao wawili hawana shida. Wa kwanza yy mpole sana na anapenda kusali,wa pili wa kiume hapendi kabisa kusali wkt wa kulala akisikia mda wa kusali anaanza kulegea mara achuchumae cha kuchekesha zaidi mwenzake huyo wa kwanza 5 yrs akianzisha sala basi yy anamfanyia alama ya dole huyu dogo ana miaka 3. Wa tatu yy ni seven months yani huyu mtt toka azaliwe siku alipoanza kuoga akishaoga hataki kuvaa kabisa analiaaa basi nikajua labda sababu ni bibi yake ndo anamvalisha kumbe ni katabia mpk leo akivuliwa nguo akioga anatuliaa sasa kimbembe wkt wa kuvaa. Lol ila raha Mungu nashukuru kwa uzao.
 
Watoto katika hatua zao za ukuaji na kujifunza wanakuwa na mambo flani flani ya kufurahisha sana yaani mwanao anaweza kukuvunja mbavu balaa.
Mfano
1. Mwanangu (1.5years) anaweza kuwa anatazama TV akisikia unaongea na simu au umeweka music kwenye simu anakimbia kuja kuangalia simu hata kama TV ilikuwa na TV program ya katuni nzuri kiasi gani[emoji23] [emoji23] [emoji23]

2. Ukitaka alale we nenda kitandani weka music kwenye simu yako atakuja mwenyewe hata kama alikuwa anakwepa kulala[emoji23]

3. Anaheshimu simu yangu kama kituo cha polisi ila ya mama yake kashaipasua ukiiona utajua mama yake anafanya kazi idara ya miamba (geology)[emoji23]

4.Kupenda safari akiona mtu anatoka tu anaanza kuaga bye bye akijua nayeye anahusika na safari[emoji23] [emoji23]

5. Chakula kikiwa tayari, kabla sijaitwa kula yeye akiona mambo yako tayari anakuja kunipigapiga mgongoni(hajajua kuongea) akiashiria msosi tayari basi ukipotezea anaenda anarudi mpaka utakapoinuka[emoji23] [emoji23]

6. Mwanangu anatabia flani kama wivu, akiona naongea na mama yake mara nimemshika mkono tunaongea kama jambo la siri anakuja fasta analia anataka mama yake ambembe[emoji23]
Nadhani hajajua kwamba mama yake ni mke wangu[emoji23] [emoji23] [emoji23]

Hivi ni baadi ya vituko vya watoto mdau ongeza vya mwanao
Watoto wanaleta raha sanaaa
View attachment 521347
a2bfcb1e695ac08456bb01a4e15eb743.jpg

amelilia peni na daftari mpaka nimempa daftar langu muhimu alichoandika sasaaa
 

Attachments

Back
Top Bottom