Viongozi CHADEMA kubalini ushauri

Viongozi CHADEMA kubalini ushauri

Wasiposhiriki wananchi hawatawaelewa (watawalaumu) na kusema kama wangeshiriki wangeweza kushinda. Lakini wskishiriki na kufanyika ubakaji kama uliofanyika, wananchi watajionea wenyewe, then wataweza kuamua wawaunge mkono namna gani. Jambo linalotakiwa ni kutafuta kuungwa mkono na wananchi, lakini chama kama chama hakiwezi kushinda bila ya kuwa na support ya wananchi. Kwa baadhi ya clips zilizorusha mtandaoni na ushahidi wa aina nyingine wananchi wanaopata clues ya mambo Chadema au vyama vya upinzani vinavyofanyiwa rough.

Sawa nimekuelewa unachosema. Ila fahamu kwamba hii sio mara ya kwanza. Wananchi wanajua mfumo upoje ila CHADEMA inalazimisha washiriki. Mimi naamini CHADEMA wangegoma kushiriki wananchi wengi wangewaunga mkono.
 
Viongozi wa chadema utawaonea tu maana hata wasingeshiriki tlp, udp na vyama vingine rafiki wangeshiriki na lawama zingekua kwa staili tofauyi tu kwamba hamjashiriki mmewapa fursa.

Mtu pekee wa kupewa lawama ni mwananchi wa tanzania
Kama Watanzania wameridhika hamna tabu. Uchaguzi ni wao. Kura zilizoibiwa ni zao.

Ukiibiwa kwa ridhaa yako, nani anastahili kukulaumu?
 
Nadhani pia chadema inatakiwa kubadilisha uongozi wa juu. Mbowe apumzike abaki kuwa mshauri ikipendeza hata Heche awe mwenyekiti na katibu awe Mwabukusi huku makamu akiendelea kuwa Lissu.

Ili kuitikisa CCM kunahitajika viongozi aggressive Mbowe ni amezeeka na ameanza kukihofia sana kifo.
 
Siku kikiibuka chama kipya chenye nguvu kipesa ambacho ni Cha kizalendo kweli kweli na sio maigizo ndio mwanzo wa chadema kukosa wafuasi

Kweli kabisa mkuu. Kuna kipindi niliandika ya kwamba CHADEMA kijifunze kutoka kwa Cha RENAMO kilichokuwa chama kikuu Cha upinzani Msumbiji. Kilibweteka kikaanza maridhiano na serikali , Leo sio Tena chama kikuu Cha upinzani watu wamekisusia wamehamia chama Cha PODEMOS
 
Kushiriki UCHAGUZI unaijua mshindi nani ni ujinga wa Karne Kila mwaka baada ya UCHAGUZI chadema ni kulalamika tu unaona wapo sawa kichwani halafu UCHAGUZI ujao wanashiriki tena
Itachukua muda, ila kushiriki kwao ndiko kutakaowafanya wananchi wawaunge mkono. Wasiposhiriki CCM itatumia huo mwanya kuwaonyesha wananchi kwamba wasichague chama kinachoogopa uchaguzi. Lakini wakishiriki na kufanyika madudu wananchi watazinduka na kusema ngoja wawaunge mkono. Hata kwenye mashindano ya michezo ni heri timu ishiriki na ifanyiwe faulo, maana mashabiki wataona, kuliko ile ambayo haishiriki maana mashabiki hawataelewa - wanahitaji waone. Kushiriki uchaguzi na kufanyiwa madudu ndiko kunskoleta support ya wananchi. Siku moja nili'share' na watu niliosoma nao kwenye group letu kwamba sijawahi kushiriki uchaguzi wowote tangu mwaka 2020. Wadau walinipakia sana, wakisema "watu wote wangekuwa kama wewe Botswana chama cha upinzani kingrdhinda?" Nikatafakari, nikaona ni kweli, maana unaweza kususia uchaguzi kumbe mwaka huo ndio wananchi wsmesmua wakuunge mkono, sasa utashindaje kama hudjiriki uchaguzi? Upo hapo?
 
Nadhani pia chadema inatakiwa kubadilisha uongozi wa juu. Mbowe apumzike abaki kuwa mshauri ikipendeza hata Heche awe mwenyekiti na katibu awe Mwabukusi huku makamu akiendelea kuwa Lissu.

Ili kuitikisa CCM kunahitajika viongozi aggressive Mbowe ni amezeeka na ameanza kukihofia sana kifo.

Kweli kabisa. Mimi naamini mwenyekiti angekuwa heche au Lissu CHADEMA isingeshiriki huo uchaguzi.
 
Itachukua muda, ila kushiriki kwao ndiko kutakaowafanya wananchi wawaunge mkono. Wasiposhiriki CCM itatumia huo mwanya kuwaonyesha wananchi kwamba wasichague chama kinachoogopa uchaguzi. Lakini wakishiriki na kufanyika madudu wananchi watazinduka na kusema ngoja wawaunge mkono. Hata kwenye mashindano ya michezo ni heri timu ishiriki na ifanyiwe faulo, maana mashabiki wataona, kuliko ile ambayo haishiriki maana mashabiki hawataelewa - wanahitaji waone. Kushiriki uchaguzi na kufanyiwa madudu ndiko kunskoleta support ya wananchi. Siku moja nili'share' na watu niliosoma nao kwenye group letu kwamba sijawahi kushiriki uchaguzi wowote tangu mwaka 2020. Wadau walinipakia sana, wakisema "watu wote wangekuwa kama wewe Botswana chama cha upinzani kingrdhinda?" Nikatafakari, nikaona ni kweli, maana unaweza kususia uchaguzi kumbe mwaka huo ndio wananchi wsmesmua wakuunge mkono, sasa utashindaje kama hudjiriki uchaguzi? Upo hapo?

Nachojua wananchi wengi wa Tanzania hawaukubali mfumo wa uchaguzi. CHADEMA wangewaunga mkono.
 
We jiulize Kila akikamatwa yaani ni kama igizo anakamatwa kibosi kabisa tena mda mwingine mpaka unaona askari wanamuogopa

Yule atupishe CHADEMA. Hata akina Halima mdee nao wanadai Mwenyekiti ndio aliwaruhusu waende bungeni.
 
Sawa nimekuelewa unachosema. Ila fahamu kwamba hii sio mara ya kwanza. Wananchi wanajua mfumo upoje ila CHADEMA inalazimisha washiriki. Mimi naamini CHADEMA wangegoma kushiriki wananchi wengi wangewaunga mkono.
Shida ya kutoshiriki ni hii. Mfano, wananchi (kila mmoja moyoni mwake anaweza akasema 'mwaka huu napiga kura ya ndiyo kwa Chadema'). Sasa Chadema isiposhiriki, unafikiri hiyo kura itakwenda kwa nani, si ni kwa CCM? Kwa sababu wananchi wakiamua kupiga kura ya ndiyo, hujui na wanaweza wakataka wakuchague mwaka huo, then wewe unasusia, na CCM Ina mbinu nyingi za kuwaaminisha wananchi jambo fulani, na vyama vingine havina. Si hata huwa unaona habari nyingi zinazotoka kwenye vyombo vya habari ni za CCM.
 
Kama Watanzania wameridhika hamna tabu. Uchaguzi ni wao. Kura zilizoibiwa ni zao.

Ukiibiwa kwa ridhaa yako, nani anastahili kukulaumu?
mimi kwa sasa naenda na hii theory kama wananchi tumekubali basi tuendelee tu
 
Ndio kulegea Kwa nati kwenyewe huko Sasa kama watu Kila siku wanakua hawana msimamo hao ni viongozi yaani unaenda kushikana mkono na mtu ambae unataka kumtoa kwenye ulaji wake hiyo inaingia akilinihapo wanajuanana ccm wanachezea akili za watanzania

Nikikumbuka Mbowe alivyosema kuwa hata msema vibaya Rais Samiah pale kwenye Mkutano wa kwanza viwanja vya furahisha Mwanza , nilidhani amelewa kumbe alikuwa anamaanisha.
 
Nachojua wananchi wengi wa Tanzania hawaukubali mfumo wa uchaguzi. CHADEMA wangewaunga mkono.
Hahaha. Wananchi wa hapa kwetu? Mhu! Hilo sina hakika nalo. Sisi tunakosa kitu kinaitwa 'political consciousness' (utambuzi/kujitambua kisiasa). Zamani tulikuwa vizuri, lakini siyo sasa.
 
Shida ya kutoshiriki ni hii. Mfano, wananchi (kila mmoja moyoni mwake anaweza akasema 'mwaka huu napiga kura ya ndiyo kwa Chadema'). Sasa Chadema isiposhiriki, unafikiri hiyo kura itakwenda kwa nani, si ni kwa CCM? Kwa sababu wananchi wakiamua kupiga kura ya ndiyo, hujui na wanaweza wakataka wakuchague mwaka huo, then wewe unasusia, na CCM Ina mbinu nyingi za kuwaaminisha wananchi jambo fulani, na vyama vingine havina. Si hata huwa unaona habari nyingi zinazotoka kwenye vyombo vya habari ni za CCM.
Mtu mwenye akili timamu chadema ikisusia UCHAGUZI ndio atafurahi sababu hamna jipya haya wamekubali kuwa kwenye UCHAGUZI Kuna kilichobadilika zaidi ya wizi wa kura na kudharirika kupata viti 1222 dhidi ya viti 22950 yaani inaonesha kabisa wizi wa halai ya juu umefanyika
 
Back
Top Bottom