Viongozi CHADEMA kubalini ushauri

Ushauri wa bure tulitoa humu na tahadhari nikiwa miongoni mwa watu wa mwanzo kabisa niliwashauri wagomee huo upuuzi tangu kwenye uandikishaji uliojaa mambo ya kishenzi.

Tofauti na hapo nilisema wasije tu na wimbo wa tumeibiwa tena huo wimbo hatuutaki tena ni miaka 30 sasa tunausikia sasa wachukue hatua.

Walitakiwa wafanye mass boycotting ya uchaguzi , wakati serikali inahamasisha watu wajiandikishe wakati zoezi lilishapoteza uhalali wake kwa kuandikisha watoto wa shule tena wa chini ya miaka 18 wao walitakiwa wawe wanatoa elimu wananchi wakagomee zoezi la kura tofauti na hapo wamepata walichostahili.

Mtu atunge mtihani, achapishe yeye, ajisimamie mwenyewe, answer guide awe nayo mwenyewe, ajisahihishe mwenyewe halafu afeli?
 
Mkuu Mimi Mbowe kwa Sasa simkubali kabisa ni kama anatumika Sana. Ingawa nimechelewa kulijua Hilo.
Nchi hii ni ya vyama vingi sio lazima umkubali Mbowe, wewe endelea kivyako
. Mbowe anakukera vipi wakati unaweza kuanzisha chana chako kikayafanya hayo unayoona ni sahihi
 
Kwa kweli kiburi Cha Viongozi wa CHADEMA kitaua chama hiki Cha CHADEMA na kitakosa watu wa kujiamini.
Mkuu 'econo', unayo haki kamili ya kuwalaumu viongozi kama ulivyo jieleza hapa na kueleweka vyema.

Pamoja na hayo yote, binafsi nabaki upande wa uamzi walio fanya viongozi wenu, wa kuamua kushiriki kwenye "uchafuzi".
Hebu nieleze mkuu 'econo' hivi kweli wewe huoni hata faida ndogo tu inayo tokana na kushiriki kwenye uchafuzi huo hadi sasa?
Wewe tokea mwanzo wa mchakato ulielewa kwamba CHADEMA ikishiriki itapata ushindi? Mbinu zote za ulaghai wa CCM na vyombo vyake ulivielewa vizuri.
CHADEMA haijajifunza chochote kutokana na yaliyo fanyika? Hiyo siyo faida kwa chama, ili kitafute njia ya kuzuia ulaghai usitokee tena mbeleni?
Wananchi na wanachama wenzenu, hawajaona yaliyo fanywa na CCM. Hamuwezi kuyatumia haya kuwahimiza wananchi wayakatae? Ushahidi huu mtaacha tu upotee hivi hivi bila kuutumia?

Kosa litakuwa kama mtashindwa kutumia udhaifu huu wa CCM kwa faida ya chama chenu na kwa faida ya Tanzania kwa ujumla.
 
Nchi hii ni ya vyama vingi sio lazima umkubali Mbowe, wewe endelea kivyako
. Mbowe anakukera vipi wakati unaweza kuanzisha chana chako kikayafanya hayo unayoona ni sahihi
Hapana.

Hata wewe haupo sawa. CHADEMA siyo ya Mbowe.
 
Usilazimishe kutoa ushauri kama haujaombwa.

Aliyekuambia CHADEMA wanahitaji ushauri wako ni nani?
Wewe ni adui wa chama hicho. Sidhani kuwa kweli upo ndani ya CHADEMA wewe.
 

..kwanini hatuilaumu serikali na Ccm waliohusika kuharibu uchaguzi?

..kwanini hatuilaumu Ccm kwa kulazimisha Tamisemi isimamie uchaguzi pamoja na kwamba sheria inakataza?

..kwanini hatuilaumu Mahakama kwa hukumu ya kibabaishaji inayotoa baraka kwa Tamisemi kusimamia uchaguzi?

..lawama dhidi ya Chadema kwa yaliyotokea naona kama hazina mashiko.
 
Ukweli mchungu na unaouma kweli ni lazima tu usemwe. Kama vile ambavyo Mh.Mbowe alivyokwisha kuahidi kuwa atajiuzuru nafasi ya M/Kiti Taifa, inampasa afanye hivyo mara moja ili kumpisha kada mwingine ambaye ataweza kukiimarisha zaidi chama na kukipa mvuto mpya.

Amekwisha kifanyia mambo mengi makubwa CDM, lkn kwa aina ya siasa zake za sasa, ni dhahiri kabisa zimepitwa na wakati na wala hazina tena mvuto kwa Watanzania waliokuwa wengi. Kwa tathmini kupitia uchaguzi huu uliopita, licha ya dosari zilizojitokeza, lkn kwa ujumla zinadhihirisha udhaifu wa kupitiliza wa CDM dhidi ya CCM.

Sijajua matokeo ya jimbo lake la Hai, ama lile la Mh. Lisu, ama mengine ya viongozi wakuu. Jambo la kujifunza hapo ni kwamba, kuishia kulia bila ya kuchukua hatua stahiki pale mnapofanyiwa dhuluma za wazi, je! nini itakuwa hatma ya kudumu ya mambo haya hasa tuelekeapo uchaguzi wa 2025?

CDM ya sasa inahitaji M/Kiti Taifa aina ya Lissu ama Heche ambaye hapepesi macho pale dhuluma ya wazi inapofantika. Tunakupenda sana Mh. Mbowe kwa yote uliyokifanyia chama, ila kutokana na matwaka ya wakati, tafadhali sana mpishe kamanda mwingine aongoze jahazi ambalo linazidi kuzama kila uchao.
 
Kweli kabisa. Mimi naamini mwenyekiti angekuwa heche au Lissu CHADEMA isingeshiriki huo uchaguzi.
Mbowe hapana ni kama anaisaidia sana CCM badala ya chama chake. Amekuwa soft mno ni kama yuko tu Ccm Lissu pamoja na uropokaji wake angalau unamuona kabisa ana machungu na chama. Heche utendaji wake kwenye Bavicha yake unampa credit ya kuwa kwenye rekodi nzuri.

Lakini pia Ccm limekuwa janga la kitaifa linatakiwa likemewe na kila mwenye nia njema kuanzia msikitini, kanisani na uraiani maana kilichoshuhudiwa uchaguzi wa serikali za mitaa ni uharamia wa ajabu sana.
 
Ua
muzi wao wa kutosusia walikuwa sahihi, maana CCM hata ukisusa wao ni mbele kwa mbele, bora uwape wakati mgumu kidogo, wangesusia mwanzoni wasingeziona hizi sarakasi zilizoendelea.
 
Mliendesha kampeni kubwa sana kwamba watu wasijiandikishe so mlitegemea mpiga kura wenu awe nani?
 
Sawa hakuna kilichobadilika, lakini hata viongozi wa dini wamefahamu mbinu chafu zinazotumika dhidi ya vyama vya upinzani. Wangesusia hizo mbinu chafu zingebaki tu kama speculation. Kususia ni njia mojawapo ya ku'disapprove' jambo, lakini si njia pekee, na pia inategemea mazingira. Hapo unasema "watu wenye akili timamu" ni wangapi wanaoiunga mkono Chadema, ukilinganisha na "wasio na akili timamu" wanaoiunga mkono Chadema pia"? Wangesusia hata hao viongozi mia kadhaa wasingepatika. Lakini tayari angalau hao wamepatikana ni starting point.
 
Mkuu unaumri Gani maana kama umeshushwa Leo duniani kwani wizi wa kura umeanza mwaka huu mpaka useme wameshafahamu si Kila mwaka wa UCHAGUZI chadema wanashiriki na wanalalamika kuibiwa kura unaona hao watu wanaakili timamu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…