Viongozi CHADEMA kubalini ushauri

Too bad kitaingia kwenye mifumo ile ile iliyowekwa na serikali na kitakuwa weaked, aka chadema 2.0

Until mifumo ya uchaguzi na mazingira yatakapo badilishwa for good, haijalish chama gani kipya kitakuja. Hakutakuwa na changes
Mifumo ya UCHAGUZI haiwezi kubadilika kama vyama vya siasa Ambavyo ni pinzani ni ccm b vyote
 
Mifumo ya UCHAGUZI haiwezi kubadilika kama vyama vya siasa Ambavyo ni pinzani ni ccm b vyote
Nope itaweza badilika kama vyama vya upinzani vitarudisha umoja na mshikamano. Hakuna wakati upinzani ulikuwa na capability ya kuleta changes kama kipind cha UKAWA.

Ccm know this is why wanapenyeza watu wao ili yasitokee
 
Hizo mbinu chafu zimeanza Leo?
 
CV ya Kwanza kabisa kwa hapa JF ni hoja mnazoandika hapa!
 
Hakuna kiongozi pale, kuna MFANYABIASHARA WA SIASA
 
Nope itaweza badilika kama vyama vya upinzani vitarudisha umoja na mshikamano. Hakuna wakati upinzani ulikuwa na capability ya kuleta changes kama kipind cha UKAWA.

Ccm know this is why wanapenyeza watu wao ili yasitokee
Kwa akili Yako unavyoona Kuna chama Cha upinzani tanzania
 
Lakini pia wananchi wenyewe hawaaminiki hata kama ni jambo linalowahusu. Nilishashiriki nikiwa Malawi kwenye kutetetea haki za wakulima wa tumbuku. Kule zao kuu la biashara ni tumbaku - matajiri na watu wakubwa wana mashamba makubwa. Sasa tulitembelea mashamba kadhaa, wakulima wakatoa malalamiko yao: malipo madogo, na yanachelewa sana hata miaka 5 mtu haijalipwa, etc. Tuliorodhesha malalamiko yao, tukawahamasisha tufanye maandamano makubwa hadi kwa mkuu wa wilaya tuliyokuwemo. Sawa kwenye maandamano walikuja kama wakulima 200 hivi. Polisi walikataza, lakini tulipuuza katazo tuakaendelea na maandamano. Tulichokifanya hata kabla polisi hawajafika kazini, tulikuwa tumeshafika ofisi ya DC, na wakulima wetu tuliwaambia wasifanye fujo yoyote, wakati wa maandamano tukae kushoto mwa barabara kuruhusu watumiaji wengine wa barabara, na hakuna kuongea na mtu au kutoa sauti inayowabugudhi wengine. Kwa hilo tulifanikiwa, hadi kufikia na tukaa chini kwa utulivu. DC alipokuja, akatuuliza "mnataka nini", tukasema tuna malalamiko tunayotaka uyasikie na uyapeleke kwa Rais. Tuliandaa risala iliyogusa maeneo yote yanayolalamikiwa. Tulikuwa pia tumewaandaa BBC wakarusha maandamano yetu hewani. Baada ya risala, DC akasema "nimesikia malalamiko yenu, nitayafanyia kazi. Rudini mlikotoka kwa amani." Tukarudi. Baada ya wiki hivi tukapokea barua (sisi waratibu), kwamba tuwapeleke viongozi kadhaa wa serikali kwenye hayo mashamba yenye malalamiko. Tukawaandaa wakulima wetu kwamba siku fulani wanatakiwa wawe mashambani kwao, maana wakuu fulani kutoka serikalini watawatembelea. Siku ya siku, hao viongozi wakaja. Tukawapeleka. Kwenye hayo mashamba hatukukuta mtu, hata baada ya kukaa muda mrefu watu wajitokeze. Hao viongozi wakatuuliza "wakulima wanaolalamika wako wapi?" Tukakosa jibu. Nao wakarudi walikotoka, na matatizo ya wakulima yakaendelea. Kwa vile wenye mashamba baadhi yao walikuwa watu wakubwa serikalini, huenda walitoa vitisho kwa tenants wao kwamba "ole wenu mtu aende kuonana na hao viongozi, nitamfukuza!" Maana tenants walikuwa wanachukuliwa kutoka mbali, sasa ukifukuzwa na una malimbikizo ya malipo unayodai hata miaka 5 au zaidi, utakubali uende kwenye mkutano kweli? Sasa hapa nimetaka nioanishe hiki walichotufanyia hawa tenants waliotupa moyo tuwapiganie wapate haki zao, lakini wakatu'disappoint' na wananchi wasiojitambua: tatizo wanaliona, lakini wameaminishwa kwamba kudai haki yao "ni kushindana na serikali...na kwamba serikali ina mkono mrefu huwezi kushindana nayo." Unaona tatizo lilipo? Hivyo, hata chama kinaweza kuibua hoja yenye public interest, lakini support ya wananchi inakuwa ndogo sana. Mfano, suala la Katiba mpya, si huwa tunasikia baadhi ya wanasiasa kutoka chama tawala wakisema "wananchi hawahitaji katiba mpya, wanachohitaji ni maji, ajira, huduma za jamii, na ona miundombinu ilivyoboreshwa, etc... Sasa katika mazingira haya, unakuta wananchi wanarudi nyuma, na kuona hao wanasiasa ndio wanaowaambia ukweli.
 
Kwa akili Yako unavyoona Kuna chama Cha upinzani tanzania
Vilikuwepo until 2015, thats when upinzani ulikufa rasmi. Ulioko sasa uko controled, waanamua washinde nafas ngapi, wapi, kwa wakati gani.
 
Vilikuwepo until 2015, thats when upinzani ulikufa rasmi. Ulioko sasa uko controled, waanamua washinde nafas ngapi, wapi, kwa wakati gani.
Ndio maana nakuambia haiwezekani kufanya hivyo ulivyosema sababu hamna upinzani Kuna maigizo Ili kuonekane Kuna demokrasia nchini sababu watanzania sisi ni waoga bila kuwa na chama Cha upinzani watu wachache tukianzisha maandamano tutaitwa magaidi na kupigwa risasi sababu sisi hatuna silaha ya kujibu ofopa sana uitwe gaidi halafu huna silaha ya kujibu sababu utachakaa Kwa risasi na wewe huna ya kujibu
 

Wananchi wakipata viongozi shupavu wa upinzani wa kuaminika, utaona jinsi equation itakavyochange.

Mbowe kesha flipflop sana hana imani ya umma. Watu wanamiona keshanunuliwa na Samia, kwa hiyo hata akiitisha mass action. watu wanampuuza.
 
Hizo mbinu chafu zimeanza Leo?
Hazikuanza leo. Je, wananchi do they lack awareness or consciousness? Kwa maoni yangu, wananchi wanajua, lakini shida ni kujitambua, na kujitambua kunachukua muda. Na ndilo tatizo lililo hapa kwetu.
 
Hazikuanza leo. Je, wananchi do they lack awareness or consciousness? Kwa maoni yangu, wananchi wanajua, lakini shida ni kujitambua, na kujitambua kunachukua muda. Na ndilo tatizo lililo hapa kwetu.
Kujitambua kwa sehemu kubwa tayari. Wananchi wengi kususia uchafuzi ni dalili mojawapo. Kinachokosekana ni UMOJA kuelekea kuchukua hatua stahiki
 
Tahrir square kulifanyika maanamano ya kumuondoa rais hosni mubarak, mwaka 2011. Raia wale hawakuwa na silaha, bali walikuwa na lengo moja
Polis waliwagonga sana, hawakurudi nyuma.
Waliitwa magaid, wakafungwa na kuuwawa


Baadhi ya nchi za africa ya kati zimefanya mapinduzi majuzi hapa? What is the difference?

Jamii ya mtanzania haina umoja. Umoja wao uko kwenye baadhi ya majanga na mambo yasiokuwa serious
 
Kujitambua kwa sehemu kubwa tayari. Wananchi wengi kususia uchafuzi ni dalili mojawapo. Kinachokosekana ni UMOJA kuelekea kuchukua hatua stahiki
Mimi sioni hivyo.
1) Kujitambua bado.
2) Hali ngumu ya maisha inafanya watu wachakalike, na mtu anaona kuliko kwenda kupiga kura, ngoja nikaingize shilingi moja, maana siwezi kula siasa.
3) Mtu aliyejitambua ataona kwamba tukiwa na viongozi bora mabadiliko chanya yatatokea kuliko hali ilivyo sasa.
4) Kwa hiyo, ataweka kipaumbele kwenye kushiriki kwake, na hatakubali haki yake ipokonywe kirahisi.
5) Asiyejitambua ni rahisi sana kupokonywa haki, na anaona hana la kufanya.
 
Kwani wewe ndiye CHADEMA auni mali yako?

Hivi huoni unavyo jionyesha kuwa juha, au mpaka uelezwe pointi kwa point jinsi ujuha wako ulivyoi?
Huoni kuwa wewe ni zaidi ya juha,!

Wewe una akili gani kuzidi strategists wa CHADEMA hadi ung'ang'anie wafuate mawazo yako.

Mimi sio mwanachama wa CHADEMA ila nakushangaa wewe unavyodhani unaweza kuwachuuza CHADEMA .
 
Kutoshiriki uchaguzi sio ufumbuzi wa tatizo.mabadilikko yakutoka kwenye ujinga kwenda kwenye werevu na ustarabu kwa sisi waafrika sio kazi ya siku moja.Hadi sasa sisi sio kizazi cha binadamu wastarabu ndo mana mambo kama haya yakijinga bado yapo,sasa hayawezi kuisha bila kuendelea kuyaweka wazi,iko siku kitapatikana kizazi cha wenye akili tofauti nazakwetu wakaamua kubadilisha historia.Pole pole tutafika tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…