Lakini pia wananchi wenyewe hawaaminiki hata kama ni jambo linalowahusu. Nilishashiriki nikiwa Malawi kwenye kutetetea haki za wakulima wa tumbuku. Kule zao kuu la biashara ni tumbaku - matajiri na watu wakubwa Wana mashamba makubwa. Sasa tulitembelewa mashamba kadhaa, wakulima wanatoa malalamiko yao: malipo madogo, na yanachelewa sana hata miaka 5 mtu haijalipwa, etc. Tuliorodhesha malalamiko yako, tukawahamasisha tufanye maandamano makubwa hadi kwa mkuu wa wilaya tuliyokuwemo. Sawa kwenye maandamano walikuja kama wakulima 200 hivi. Polisi walikataza, lakini tulipuuza katazo tuakaendelea na maandamano. Tulichojifanya hata kabla polisi hawajafika kazini, tulikuwa tumeshafika ofisi ya DC, na wakulima wetu tuliwaambia wasifanye fujo yoyote, wakati wa maandamano tukae kushoto mwa barabara kuruhusu watumiaji wengine wa barabara, na hakuna kuongea na mtu au kutoa sauti inayowabugudhi wengine. Kwa hilo tulifanikiwa, hadi kufikia na tukaa chini kwa utulivu. DC alipokuwa, akatuuliza "mnaotaka nini", tukasema tuna malalamiko tunayotaka uyasikie na uyapeleke kwa Rais. Tuliandaa risala iliyogusa maeneo yote yanayolalamikiwa. Tulikuwa pia tumewaandaa BBC wakarusha maandamano yetu hewani. Baada ya risala, DC akasema "nimesikia malalamiko yenu, nitayafanyia kazi. Rudini mlikotoka kwa amani." Tukarudi. Baada ya wiki hizi tukapokea barua (sisi waratibu), kwamba tuwapeleke viongozi kadhaa wa serikali kwenye hayo mashamba yenye malalamiko. Tukawaandaa wakulima wetu kwamba siku fulani wanatakiwa wawe mashambani kwao, maana wakuu fulani kutoka serikalini watawatembelea. Siku ya siku, hao viongozi wakaja. Tukawapeleka. Kwenye hayo mashamba hatukukuta mtu, hata baada ya kukaa muda mrefu watu wajitokeze. Hao viongozi wakatuuliza "wakulima wanaolalamika wako wapi?" Tukakosa jibu. Nao wakarudi walikotoka, na matatizo ya wakulima yakaendelea. Kwa vile wenye mashamba baadhi yao walikuwa watu wakubwa serikalini, huenda walupeleka vitisho kwa tenants wao kwamba "ole wenu mtu aende kuonana na hao viongozi, nitamfukuza!" Maana tenants walikuwa wanachukuliwa kutoka mbali, sasa ukifukuzwa na una malimbikizo ya malipo unayodai hata miaka 5 au zaidi, utamkubali uende kwenye mikutano kweli? Sasa hapa nimetaka nioanishe hiki walichotufanyia hawa tenants waliotupa moyo tuwapiganie wapate haki zao, lakini wakatu'disppoint' na wananchi wasiojitambua: tatizo wanaliona, lakini wameaminishwa kwamba kudai haki yao "ni kushindana na serikali...na kwamba serikali Ina mkono mrefu huwezi kushindana nayo." Unaona tatizo lilipo? Hivyo, hata chama kinaweza kuibua hoja yenye public interest, lakini support ya wananchi inakuwa ndogo sana. Mfano, suala la Katiba mpya, si huwa tunasikia baadhi ya wanasiasa kutoka chama tawala wakisema "wananchi hawahitaji Katiba mpya, wanachohitaji ni maji, ajira, huduma za jamii, na ona miundombinu ilivyoboreshwa, etc... Sasa katika mazingira hayo, unakuta wananchi wanarudi nyuma, na kuona hao wanasiasa ndio wanaowaambia ukweli.