econonist
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 20,189
- 29,663
Pamoja na uchafuzi uliofanyika, ningependa kuwasii Viongozi wa CHADEMA wawe wasikivu na kusikiliza ushaurii. Mwanzoni nilishauri tusishiriki kwenye huu uchaguzi wa Serikali za mitaa baada ya mahakama kubariki TAMISEMI kusimamia uchaguzi huo. Kila Mtendaji kapewa maelekezo ya kufanya Sasa unategemea Nini?
Ila Viongozi wa CHADEMA wanajua na msimamo wa kushiriki uchaguzi huo. Nikawa najiuliza je Viongozi wanamkakati wa kuzuia hujuma za CCM? Wagombea wakaenguliwa na vituko vingi kufanya, lakini bado Viongozi wakaendelea kushiriki huo uchaguzi. Najiuliza kwa Yale yaliyotokea kulikuwa hakuna haja ya kuendelea na huo uchaguzi, ilibidi chama kijitie kuonesha protest ya udhalimu uliofanyika.
Mwisho wa siku Viongozi wamelazimisha kushiriki uchaguzi na wakaingia kwenye mtego wa CCM. Maana hata wakiiba utafanya Nini wakati polisi wapo upande wao? CCM wamefanya Hila nyingi kwenye uchaguzi huu lakini kwao ni kawaida.
Hasa Viongozi wamebakia kulalamika na kulaumu. Kwani mlitegemea uchaguzi unasimamiwa na kada wa CCM na Tena mkwe wa Rais awatendee haki. Nilishangaa Sana Lema aliposusia uchaguzi siku ya kupiga kura, nikajiuliza unasusia uchaguzi mwishoni kwanini? Akazira hata kufuatilia matokeo. Nikashangaa Wenje anashadadia CHADEMA ishiriki, nikashangaa Kuna jipya lipi ambalo lipo Kwa CCM linalowafanya Viongozi washiriki uchaguzi huu?
Kwa kweli kiburi Cha Viongozi wa CHADEMA kitaua chama hiki Cha CHADEMA na kitakosa watu wa kujiamini.