Mpaka hapa uko sawa.
Ila ukweli halisi ni kuwa hana bifu na TISS Kwa ujumla wake bali na baadhi tu ya viongozi wake hususani aliyekuwa DG wao ambaye sasa ni balozi somewhere huko nchi za kigeni
Ndugu
Huihui2 ni wazi huna taarifa sahihi na za kutosha juu ya mgogoro huu kati ya mchungaji huyu na polisi/serikali.
Iko hivi;
1. Huyu ndugu humtaja aliyekuwa DG wa TISS direct kuwa ndiye aliyeua mwanae. Kama tuhuma ziko direct kiasi hiki kwa muhusika tena akitajwa kwa jina lake, tunadhani ni kwanini mamlaka na vyombo husika havichukui hatua? Au ni haki kwa kiongozi kuua?
2. Na kabla ya hapo upo mgogoro wa kukataliwa kusajiliwa kwa taasisi/kanisa lake licha ya kufuata taratibu zote ikiwemo kuwasilisha nyaraka zote zunazotakiwa kisheria. Amefuatilia Dodoma na DSM miaka na miaka mpaka kachoka. Ameingia kila mlango wa ofisi ya serikali lakini yote imefungwa, hapati msaada na hasikilizwi. Njia pekee aliyobaki nayo kupambania haki yake ni mdomo......yaani kupiga kelele na kusema kila kitu
3. Haya yakiwa yanaendelea, akawa amefunguliwa kesi mahakama ya Mbeya. Kwa maelezo yake ni kuwa hata huko mahakamani watesi wake hapa wameshafika na wameikamata mahakama ili tu kuhakikisha hapati anachokitaka..!
##
Katika mazingira haya kwanini mtu asifikiri kuwa labda yeye na watu wake wanaonekana ni manyani (wanyama) tu wasiostahili kutendewa kama wanadamu?
1. Hueleweki ndugu
Huihui2. Wanamshauri kitu gani kama yule anayesemekana ameua mtoto wake yupo analindwa na kutamba mitaani? Hapa si ishu ya kishauri bali ni sheria kuchukua mkondo wake.
2. Wanafanya kiburi gani? Unataka waunyamazie na kuunyenyekea uovu na waovu?
Kama hawa watumishi wa Mungu wanachofanya ni kukemea matendo maovu, wizi, uonevu, ufisadi na kutowajibika Kwa viongozi wenye dhamana serikali unatafsiri kama "kuoneshana umwamba na serikali", basi huu umwamba Kila mpenda HAKI ni lazima auonge mkono..
Hujui usemalo na huijui historia ya kanisa wewe. Nitakupa mifano michache toka kwenye Biblia..
1. Unamjua Mfalme (Rais) wa kwanza kutawala wanadamu aliyeitwa Sauli wakati wa utumishi wa Mungu Nabii Samweli? Unajua nini kilimtokea Mfalme huyu baada ya serikali yake kuwa ya mabavu na kuonea watu huku yeye mwenyewe Mfalme akimkufuru Mungu ktk kiwango cha kutisha sana? Kama hujui, nakuambia kuwa utawala wake ulianguka na yeye mwenyewe Mfalme Sauli kufutiliwa mbali (kufa) kwa sababu ya maombi ya Nabii Samweli. [Soma kisa hiki kwenye Biblia yako kitabu
cha 1 Samweli 15:1 - 35]
2. Pia
soma 1 Wafalme 18:1-46 utakutana na kisa kilichorekodiwa cha mtumishi wa Mungu Nabii Eliya dhidi ya utawala wa Mfalme (Rais) Ahabu na mkewe Malkia Yezebel waliokuwa wanatawala nchi na watu kwa kutumia nguvu za miungu iliyoitwa Baali na kuleta mateso na mahangaiko kwa wananchi na watumishi wengi wa Mungu. Kanisa likiwakilishwa na Mtumishi wa Mungu Nabii Eliya lilisimama imara na kuukemea uovu huo. Utawala wa Ahabu ulianguka yeye na mkewe wakafyekelewa mbali..
3. Soma pia kisa cha Mfalme Farao [soma Biblia yako kitabu cha
Kutoka sura 4 - 10 na mkazo zaidi sura ya 11] wa Misri ya kale alivyokuwa na kiburi na kutesa na kuwadharau watumishi wa Mungu Lakini kwa maombi na sala za watumishi wa Mungu, utawala wake ulianguka na kupotea mpaka leo yeye mwenyewe na jeshi lake lote na silaha zake nzitonzito kama vile, magari ya washawasha, mabomu ya machozi, bunduki na vifaru walifia na kuzikwa chini ya vilindi vya bahari ya Shamu mpaka leo.
Point hapa ni kuwa si kweli kuwa hakuna serikali iliyowahi kuangushwa na maombi ya watumishi wa Mungu BALI kinyume chake ni kuwa, hakuna serikali yoyote duniani ambayo iliwahi kupambana na kanisa la Mungu aliye hai (au sema watumishi wa Mungu) na serikali ikabaki salama, imesimama..!!
Na Tanzania mgogoro huu unaoendelea kati ya KANISA na serikali, hakika anguko la serikali liko wazi kuliko unavyofikiri..!