samesame
Senior Member
- Jul 21, 2019
- 143
- 324
Baada ya kutokea kifo cha Hayati Magufuli, kumekuwa na mitizamo tofauti tofauti juu ya uongozi wake. Upande mmoja ukisema Magufuli alikuwa anaongoza nchi vizuri sana wengine wakisema aliongoza nchi vibaya vibaya mno!
Hawa hapa ni baadhi ya viongozi wa Serikali na wa Chama cha Mapinduzi waliosema alikuwa anaongoza nchi vibaya sana. Kwa lugha nyepesi wanafurahi kwa mabadiliko haya ya kiuongozi japo wanasikitika kwa binadamu mwenzetu kufariki dunia.
1: Stephen Wasira alikuwa akihojiwa na tv moja akasema nchi sasa ina furaha. Furaha imeongezeka miongoni mwa Watanzania kwa utawala mpya. Hiyo ina maana nchi ilikuwa kwenye huzuni kubwa.
2: Mwanasheria Mkuu Mstaafu, Jaji Werema akasema sio siri kwamba tulikuwa na utawala ambao wote tuliufyata, sasa tunapaswa kuwa na Katiba Mpya itakayompa kila mtu uhuru, sio hii iliyompa kila kitu mtu mmoja kuamua kila kitu.
3: Anthony Diallo, huyu ndio alienda mbali sana na kusema tulimkabidhi nchi mtu aliyekuwa na faili Milembe. Biashara zikavurugika. Kiukweli tulikuwa na hali mbaya. Na kushauri huko mbele tusirudie.
4: GAG msitaafu Profesa Assad akasema suala la Katiba Mpya halizuiliki tunaweza kupishana lini ipatikane lakn ni la lazima kwasababu tumetoka kwenye utawala uliovunja katiba kwa hali ya juu. Hivyo tunapaswa kujenga taasisi imara za kudhibiti viongozi.
5: Huyu wa tano nimuweke mama la mama. Yeye huwa hasemi ila anasema kwa vitendo. Kaingia tu na kusema TRA mlikuwa mnabambikia kodi ovyo.
Polisi mlikuwa mnabambikia kesi za uongo futeni. Taasisi ya kuzuia rushwa nanyi hamkuwa mbali.
Pesa zilizoporwa na TRA zirudishwe, sijui kesi za uhujumu uchumi na wale walioonewa warudishiwe pesa zao. Viongozi wasiofata miiko ya kazi tupa kule kamtolea mfano Sabaya. Mama anaupiga mwingi ila hasemi nani aliyekuwa anapoteza pasi zisifike uwanja mzima.
Wapo na wengine wengi ukiachilia mbali akina sisi tusio na majina. Tunafuraha kwa mabadiriko haya ya kiuongozi yameleta nuru baada ya giza nene. Hata wawekezaji wamesema sasa tunaweza kuja kuwekeza baada ya kuondoka yule na kuja huyu. Hili alilisema Aliko Dangote.
Je, wewe uko upande gani?
Pia tunaweza kuweka na maoni ya viongozi wengine zaid ya hawa.