Viongozi hawa wamesema Hayati Magufuli aliongoza nchi vibaya sana, wewe je?

Viongozi hawa wamesema Hayati Magufuli aliongoza nchi vibaya sana, wewe je?

Kiukweli wote wameongea kweli tupu, na kwa uchache wao wanawakilisha kundi kubwa sana! Ukitaka kujua ukweli wa hilo fuatilia matukio ya namna watu katika sehemu mbalimbali walivyopokea kwa shangwe taarifa za kifo cha mwendazake, lait kama yale matukio yote yangerushwa kwenye vyombo vya habari ndipo watu wangejua ni jinsi gani mwendazake alikuwa na maadui wengi aliojitengeezea mwenyewe kwa maneno na matendo!
 
Wajinga walioishi katika ujinga na unafiki, wangeweza kumchagua Magufuli, lakini yeye mwenyewe alikuwa anajua kuwa kwenye uchaguzi wa haki asingechahuliwa, ndiyo maana aliamua kuharibu uchaguzi.

Mtu kama una akili timamu, ungempa Magufuli kura kwa sababu gani?

1) Uchumi aliuharibu kwa kiwango cha hali ya juu

2) Demokrasia aliichafua kwa namna ya ajabu

3) Haki za raia alizikanyaga kwa nna ambayo haijawahi kushuhudiwa

4) Uhuru wa vyombo vya habari aiuua

5) Umoja wa kitaifa aliutekeza kwa kuendekeza upendeleo na ubaguzi

6) Haki za watu za kuishi hakuziheshimu. Kwa kutumia magenge ya wauaji aliwau, kutrka na kupoteza kila ambaye alimkosoa kwa uwazi

7) Mahusiano mazuri ya kimataifa aliyoyakuta aliyanyongelea mbali akaendekeza primitive politics
Hayo yote uliyoyaandika hvi unahisi tanzania ingelikuwa HV.siku mkitawaliwa na dicteta si mtasema magufuli alikuwa mwema sana.IPO siku mtamkumbuka ,ni mda tuu ndio utatupa jibu
 
Hii nchi mpaka kumchagua mbarubaru majnuni yule mara mbili inaonekana tuna tatizo kubwa sana.

Nyie si ndomlisema mnataka nchi ichukueliwe na jeshi. Au mmesahau jinsi mlivyokuwa mkimtukana mzee mtanashati Kikwete. Kweli nimeamini kwa binadamu hamna jema. Ndiyo maana aliyewaumba kaamua awaangalie tu mnavyojivuluga.
 
Unaposema "nyie" unamaanisha kundi gani? Na mimi unanihusishaje na kundi hilo?

Mimi niliwahi kusema hivyo lini?

Mbona kama unaniunganisha na kundi nisilolijua kwa kauli ambayo sijaisema?

Unaweza kunipa nukuu ya maneno yangu mwenyewe niliposema hivyo ili tujue kwamba nilisema maneno hayo kweli na hujanisingizia tu kwa uongo?
 
Unapozema "nyie" unamaanisha kundi gani? Na mimi unanihusishaje na kundi hilo?

Usiwe muoga hivyo Kiranga. Kuna kundi kubwa la waTanzania (kama wewe haukuwa miongoni mwao naomba nisamehe bure) waliokuwa wakitamani sana nchi pendwa Tanzania ichukuliwe na jeshi. Hilo nina imani kuwa unalikumbuka.
 
Hakuna mantiki yeyote .....
 
Usiwe muoga hivyo Kiranga. Kuna kundi kubwa la waTanzania (kama wewe haukuwa miongoni mwao naomba nisamehe bure) waliokuwa wakitamani sana nchi pendwa Tanzania ichukuliwe na jeshi. Hilo nina imani kuwa unalikumbuka.
Usiunganishe watu kijumlajumla.
 
Baada ya kutokea kifo cha Hayati Magufuli, kumekuwa na mitizamo tofauti tofauti juu ya uongozi wake. Upande mmoja ukisema Magufuli alikuwa anaongoza nchi vizuri sana wengine wakisema aliongoza nchi vibaya vibaya mno!

Hawa hapa ni baadhi ya viongozi wa Serikali na wa Chama cha Mapinduzi waliosema alikuwa anaongoza nchi vibaya sana. Kwa lugha nyepesi wanafurahi kwa mabadiliko haya ya kiuongozi japo wanasikitika kwa binadamu mwenzetu kufariki dunia.

1: Stephen Wasira alikuwa akihojiwa na tv moja akasema nchi sasa ina furaha. Furaha imeongezeka miongoni mwa Watanzania kwa utawala mpya. Hiyo ina maana nchi ilikuwa kwenye huzuni kubwa.

2: Mwanasheria Mkuu Mstaafu, Jaji Werema akasema sio siri kwamba tulikuwa na utawala ambao wote tuliufyata, sasa tunapaswa kuwa na Katiba Mpya itakayompa kila mtu uhuru, sio hii iliyompa kila kitu mtu mmoja kuamua kila kitu.

3: Anthony Diallo, huyu ndio alienda mbali sana na kusema tulimkabidhi nchi mtu aliyekuwa na faili Milembe. Biashara zikavurugika. Kiukweli tulikuwa na hali mbaya. Na kushauri huko mbele tusirudie.

4: GAG msitaafu Profesa Assad akasema suala la Katiba Mpya halizuiliki tunaweza kupishana lini ipatikane lakn ni la lazima kwasababu tumetoka kwenye utawala uliovunja katiba kwa hali ya juu. Hivyo tunapaswa kujenga taasisi imara za kudhibiti viongozi.

5: Huyu wa tano nimuweke mama la mama. Yeye huwa hasemi ila anasema kwa vitendo. Kaingia tu na kusema TRA mlikuwa mnabambikia kodi ovyo.

Polisi mlikuwa mnabambikia kesi za uongo futeni. Taasisi ya kuzuia rushwa nanyi hamkuwa mbali.

Pesa zilizoporwa na TRA zirudishwe, sijui kesi za uhujumu uchumi na wale walioonewa warudishiwe pesa zao. Viongozi wasiofata miiko ya kazi tupa kule kamtolea mfano Sabaya. Mama anaupiga mwingi ila hasemi nani aliyekuwa anapoteza pasi zisifike uwanja mzima.

Wapo na wengine wengi ukiachilia mbali akina sisi tusio na majina. Tunafuraha kwa mabadiriko haya ya kiuongozi yameleta nuru baada ya giza nene. Hata wawekezaji wamesema sasa tunaweza kuja kuwekeza baada ya kuondoka yule na kuja huyu. Hili alilisema Aliko Dangote.

Je, wewe uko upande gani?

Pia tunaweza kuweka na maoni ya viongozi wengine zaid ya hawa.
Ongeza list Samia, kigwangala, kikwete, Nape, Ndugai.

Sasa kama hawa waliokuwa wanalipwa na kula pesa kutoka kwake wanasema hivi mimi mchuuza dagaa hapa soko la Kibaigwa nitasemaje?
 
Back
Top Bottom