Viongozi hawa wamesema Hayati Magufuli aliongoza nchi vibaya sana, wewe je?

Wajinga walioishi katika ujinga na unafiki, wangeweza kumchagua Magufuli, lakini yeye mwenyewe alikuwa anajua kuwa kwenye uchaguzi wa haki asingechahuliwa, ndiyo maana aliamua kuharibu uchaguzi.

Mtu kama una akili timamu, ungempa Magufuli kura kwa sababu gani?

1) Uchumi aliuharibu kwa kiwango cha hali ya juu

2) Demokrasia aliichafua kwa namna ya ajabu

3) Haki za raia alizikanyaga kwa nna ambayo haijawahi kushuhudiwa

4) Uhuru wa vyombo vya habari aiuua

5) Umoja wa kitaifa aliutekeza kwa kuendekeza upendeleo na ubaguzi

6) Haki za watu za kuishi hakuziheshimu. Kwa kutumia magenge ya wauaji aliwau, kutrka na kupoteza kila ambaye alimkosoa kwa uwazi

7) Mahusiano mazuri ya kimataifa aliyoyakuta aliyanyongelea mbali akaendekeza primitive politics
Kwenye uchaguzi huru watanzania wangemshangaza sana
 
Tuweke kumbukumbu sawa hapa, kabla JPM hajawa mwenyekiti wa chama kunawazee walikuwa wanaamini kabisa kwamba ccm ni yakwao na wanaweza kufanya lolote walitakalo ndani ya chama.

JPM alipokabidhiwa uenyekiti akaanza kwa kuiua hiyo dhana na hilo likawa kosa kwa hao wachache uliowataja japo siamini kama wote walikuwa viongozi ndani ya chama.

Ninamawazo tofauti na wewe kuhusu mama yetu. Unawezaje kuutangazia umma kwamba nae alikuwa kwenye kundi la hao uliowataja? Mimi nadhani yeye anaongoza kwa namna anavyoona inafaa kutufikisha tunapopataka. Hakuna sheria inayomfunga kutumia mbinu za mtangulizi wake.
Dawa yenu nu katiba mpya na tumr huru.

Hii nchi ni yetu sote
 
Baada ya kutokea kifo cha Hayati Magufuli, kumekuwa na mitizamo tofauti tofauti juu ya uongozi wake. Upande mmoja ukisema Magufuli alikuwa anaongoza nchi vizuri sana wengine wakisema aliongoza nchi vibaya vibaya mno!

Hawa hapa ni baadhi ya viongozi wa Serikali na wa Chama cha Mapinduzi waliosema alikuwa anaongoza nchi vibaya sana. Kwa lugha nyepesi wanafurahi kwa mabadiliko haya ya kiuongozi japo wanasikitika kwa binadamu mwenzetu kufariki dunia.

1: Stephen Wasira alikuwa akihojiwa na tv moja akasema nchi sasa ina furaha. Furaha imeongezeka miongoni mwa Watanzania kwa utawala mpya. Hiyo ina maana nchi ilikuwa kwenye huzuni kubwa.

2: Mwanasheria Mkuu Mstaafu, Jaji Werema akasema sio siri kwamba tulikuwa na utawala ambao wote tuliufyata, sasa tunapaswa kuwa na Katiba Mpya itakayompa kila mtu uhuru, sio hii iliyompa kila kitu mtu mmoja kuamua kila kitu.

3: Anthony Diallo, huyu ndio alienda mbali sana na kusema tulimkabidhi nchi mtu aliyekuwa na faili Milembe. Biashara zikavurugika. Kiukweli tulikuwa na hali mbaya. Na kushauri huko mbele tusirudie.

4: GAG msitaafu Profesa Assad akasema suala la Katiba Mpya halizuiliki tunaweza kupishana lini ipatikane lakn ni la lazima kwasababu tumetoka kwenye utawala uliovunja katiba kwa hali ya juu. Hivyo tunapaswa kujenga taasisi imara za kudhibiti viongozi.

5: Huyu wa tano nimuweke mama la mama. Yeye huwa hasemi ila anasema kwa vitendo. Kaingia tu na kusema TRA mlikuwa mnabambikia kodi ovyo.

Polisi mlikuwa mnabambikia kesi za uongo futeni. Taasisi ya kuzuia rushwa nanyi hamkuwa mbali.

Pesa zilizoporwa na TRA zirudishwe, sijui kesi za uhujumu uchumi na wale walioonewa warudishiwe pesa zao. Viongozi wasiofata miiko ya kazi tupa kule kamtolea mfano Sabaya. Mama anaupiga mwingi ila hasemi nani aliyekuwa anapoteza pasi zisifike uwanja mzima.

Wapo na wengine wengi ukiachilia mbali akina sisi tusio na majina. Tunafuraha kwa mabadiriko haya ya kiuongozi yameleta nuru baada ya giza nene. Hata wawekezaji wamesema sasa tunaweza kuja kuwekeza baada ya kuondoka yule na kuja huyu. Hili alilisema Aliko Dangote.

Je, wewe uko upande gani?

Pia tunaweza kuweka na maoni ya viongozi wengine zaid ya hawa.
Hivi nani anaweza dhani Samia anaweza kumfuta kazi mtu kama January? Au Nape? Sioni kitu kama hiki kwa Samia.
 
Nisiunganishe watu kiujumlajumla na nani?
Sema usiniunganishe.
Usivamie watu, kama ulivyonivamia mimi, na kuwajumuisha kijumlajumla.

Ukimvamia mtu na kusema kasema hivi, akikuuliza lini, wapi, kwa nukuu ipi, unatakiwa uweze kumpa hiyo nukuu.

Bila hivyo utakuwa mtu mzushi na muongo.
 
Tupe maoni yako Kwanza ili tuende sawa,sii kutupa mawazo ya wengine tuu.
 
Mtasemaaa weee ila ukweli mnaujuaaa. Maumivuu yanawaingiaaa tartibu. Mafisadi yanavyoanza kurudii, bei za mafuta kupanda. Zambia wanapitisha hapa hapa mafuta ila kwao bei chini hapa kwa mwigulu bei iko juu.

Sara msafiri kagundua uwizi wa mafuta kigamboni kesho yake kahamishwaa na ukuu wa willayaa.

Makusanyo ya kodi yameshukaa kwa kuwabembelezaa mafisadi walipe kodi.

Subiri tuu chamoto utakipata mana ww pia unaenda dukani.

Time will tell jooombaa.
Wakwamia mahali fulani poleni wote,na tuianze safari mpya kwashida na raha tuyakubali yote.
 
Kama ni mwendawazimu, basi mpuuzeni msimuongelee. Lkn a wapi. mnachoonga juu yake na kufanya apae juu.
Maajabu ya Dunia lazima yaongelewe, SHUJAA anafaili Mirembe . Ushangai wewe..
 
Usivamie watu, kama ulivyonivamia mimi, na kuwajumuisha kijumlajumla.

Ukimvamia mtu na kusema kasema hivi, akikuuliza lini, wapi, kwa nukuu ipi, unatakiwa uweze kumpa hiyo nukuu.

Bila hivyo utakuwa mtu mzushi na muongo.

wee ni nani bana mpaka tusikuvamie mzima mzima???
 
Wewe lazima uni vamie mzimamzima kwa sababu hiyo ndiyo strategy yako ya kupata kick.

Yani mimi kukujibu ushafanya mtaji.
 
Kila watu wanapojaribu kuchunguza kama kuna uwepo halisi wa "legacy" wanapata majibu yenye utata. Mwisho wanajikuta wanakubaliana na kauli pinzani ya "tuna Rais wa ajabu kuwahi kupata kutokea hapa nchini toka nyakati za uhuru" ama ile ya "nchi kuongozwa na washamba na malimbukeni"
tapatalk_1564750429057.jpg
tapatalk_1563704539567.jpg
 
Back
Top Bottom