Viongozi hawa wamesema Hayati Magufuli aliongoza nchi vibaya sana, wewe je?

Viongozi hawa wamesema Hayati Magufuli aliongoza nchi vibaya sana, wewe je?

Kwa mafanikio mengi aliyapata, ni wazi aliiweza nchi, sema njia ya maendeleo sio kila mtu anaiweza
 
Baada ya kutokea kifo cha Hayati Magufuli, kumekuwa na mitizamo tofauti tofauti juu ya uongozi wake. Upande mmoja ukisema Magufuli alikuwa anaongoza nchi vizuri sana wengine wakisema aliongoza nchi vibaya vibaya mno!

Hawa hapa ni baadhi ya viongozi wa Serikali na wa Chama cha Mapinduzi waliosema alikuwa anaongoza nchi vibaya sana. Kwa lugha nyepesi wanafurahi kwa mabadiliko haya ya kiuongozi japo wanasikitika kwa binadamu mwenzetu kufariki dunia.

1: Stephen Wasira alikuwa akihojiwa na tv moja akasema nchi sasa ina furaha. Furaha imeongezeka miongoni mwa Watanzania kwa utawala mpya. Hiyo ina maana nchi ilikuwa kwenye huzuni kubwa.

2: Mwanasheria Mkuu Mstaafu, Jaji Werema akasema sio siri kwamba tulikuwa na utawala ambao wote tuliufyata, sasa tunapaswa kuwa na Katiba Mpya itakayompa kila mtu uhuru, sio hii iliyompa kila kitu mtu mmoja kuamua kila kitu.

3: Anthony Diallo, huyu ndio alienda mbali sana na kusema tulimkabidhi nchi mtu aliyekuwa na faili Milembe. Biashara zikavurugika. Kiukweli tulikuwa na hali mbaya. Na kushauri huko mbele tusirudie.

4: GAG msitaafu Profesa Assad akasema suala la Katiba Mpya halizuiliki tunaweza kupishana lini ipatikane lakn ni la lazima kwasababu tumetoka kwenye utawala uliovunja katiba kwa hali ya juu. Hivyo tunapaswa kujenga taasisi imara za kudhibiti viongozi.

5: Huyu wa tano nimuweke mama la mama. Yeye huwa hasemi ila anasema kwa vitendo. Kaingia tu na kusema TRA mlikuwa mnabambikia kodi ovyo.

Polisi mlikuwa mnabambikia kesi za uongo futeni. Taasisi ya kuzuia rushwa nanyi hamkuwa mbali.

Pesa zilizoporwa na TRA zirudishwe, sijui kesi za uhujumu uchumi na wale walioonewa warudishiwe pesa zao. Viongozi wasiofata miiko ya kazi tupa kule kamtolea mfano Sabaya. Mama anaupiga mwingi ila hasemi nani aliyekuwa anapoteza pasi zisifike uwanja mzima.

Wapo na wengine wengi ukiachilia mbali akina sisi tusio na majina. Tunafuraha kwa mabadiriko haya ya kiuongozi yameleta nuru baada ya giza nene. Hata wawekezaji wamesema sasa tunaweza kuja kuwekeza baada ya kuondoka yule na kuja huyu. Hili alilisema Aliko Dangote.

Je, wewe uko upande gani?

Pia tunaweza kuweka na maoni ya viongozi wengine zaid ya hawa.
Acha uchonganishi mkuu.
 
Ila Diallo ndio kapitiliza kabisa....khaaa! Ati JPM alikuwa na faili mirembe? Hasa ukizingatia nafasi ya Diallo katika ccm.....hizo ni allegations kubwa sana. Kweli watu walichoka!
 
Angekuepo wangesema analazimisha watu wampaishe
Sasa bahati nzuri wanaodhani wanamshusha ndio wanazidi kumpaisha
Ukiwa mwendawazimu, ukiambiwa wewe ni jambazi hatari, unaweza kufurahi na kutamba mbele ya majambazi wenzio kwa sababu umetambulika kuwa wewe ni jambazi hatari kuwazidi wengine.

Marehemu alifanya maovu mengi, lakini itoshe kumsamehe kutokana na tatizo lake la akili. Wa kulaumiwa ni wale waliokuwa wazima, hasa Kikwete na Mkapa, ambao walijua kabisa tatizo la akili alilokuwa nalo marehemu. Milembe alienda kutibiwa mwenyewe lakini Ujerumani, ni Mkapa ndiye aliyemlazimisha kuwa akatibiwe maana marehemu alikuwa anagoma, na kudai kuwa ni mzima, na hiyo ni kawaida kwa wagonjwa wote wa akili, huwq hawakubali kuwa wana matatizo ya akili.
 
JPM anaupiga mwingi akiwa kalala zake Chato kwa amani. Ukitaka kaumaarufu kama nyota yako kisiasa imebuma itisha press ongea ovyo kuhusu JPM hapohapo unapata dakika 15 zako za umaarufu. JPM bado yupo nasi sana topic zake hazitaisha. Actually it is very satisfying kuona mtu anakurupuka tokea mafichoni na kuanza kubwabwaja JPM was this JPM was that..hapo najua ngosha kumbe alikuwa really on the driving seat kuendesha nchi bila kutizama nyani usoni asije vuna mabua. Long live comrade JPM's name.
 
Wanazidi kumuweka juu juu bila wenyewe kujua.
[emoji7][emoji7][emoji7]
Ni kweli, kwa maana Hitler, Idd Amin, Mussolin, Pinochet kwa kutajwa sana kwa ukatili wao, wapo juu sana.
 
Wajinga walioishi katika ujinga na unafiki, wangeweza kumchagua Magufuli, lakini yeye mwenyewe alikuwa anajua kuwa kwenye uchaguzi wa haki asingechahuliwa, ndiyo maana aliamua kuharibu uchaguzi.

Mtu kama una akili timamu, ungempa Magufuli kura kwa sababu gani?

1) Uchumi aliuharibu kwa kiwango cha hali ya juu

2) Demokrasia aliichafua kwa namna ya ajabu

3) Haki za raia alizikanyaga kwa nna ambayo haijawahi kushuhudiwa

4) Uhuru wa vyombo vya habari aiuua

5) Umoja wa kitaifa aliutekeza kwa kuendekeza upendeleo na ubaguzi

6) Haki za watu za kuishi hakuziheshimu. Kwa kutumia magenge ya wauaji aliwau, kutrka na kupoteza kila ambaye alimkosoa kwa uwazi

7) Mahusiano mazuri ya kimataifa aliyoyakuta aliyanyongelea mbali akaendekeza primitive politics
Siku akili zikiwakaa vizuri[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
 
Huko paradiso anaweza kuwepo Azory Gwanda na Ben Sanane pia?
"Hata kama dhambi zenu ni nyekundu,nitazisafisha zitakuwa nyeupe kama theluji"
Hakuna aliyemkamilifu chini ya jua,kama rais wangu alipata wasaa wa kutubu na kufanya ibada kabla Israel hajainyakua rohoni yake,basi naamini rais wangu yuko sehemu salama kabisa!!.
 
Angekuepo wangesema analazimisha watu wampaishe
Sasa bahati nzuri wanaodhani wanamshusha ndio wanazidi kumpaisha
Kama kutuhumiwa kwamba alikuwa na faili Mirembe ndio kupaishwa basi hata na wewe pia hamnazo! 😂
 
Magufuli hata wamnenee mabaya vipi Ila ni Rais pekee aliyeweza kuirudisha Tanzania kwenye uwajibikaji na uadirifu. Kamwe hakucheka na kima wanaoharibu shamba.
Wanaolialia ni walewale kima wenye nia ovu na nchi hii.
waliojimilikisha nchi na Chama. Tusubiri na tuone yajayo yanachekesha na kututia aibu km nchi huru.
Pumzika Kwa amani John Pombe Magufuli
 
Namsikiliza Waziri mkuu mstaafu Judge Warioba, aisee kweli tumepita kipindi kigumu.
 
Mm hata sielewi nini kinaendelea sasa hivi,kila nikijaribu kuangalia naona giza.
 
Back
Top Bottom