KERO Viongozi kisarawe wanaisahau sana barabara ya Kiluvya Madukani-Makurunge

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Barabara ya Kiluvya Madukani mpaka Makurunge imeachwa bila matengenezo licha ya eneo hili kupata wakazi wengi miaka ya hivi karibuni.

Shida kuu:
1. Miundombinu mibovu: Barabara ni ya udongo wa mfinyanzi. Wakati wa mvua inakuwa na mashimo na inateleza sana. Magari yanakwama.
2. Ufumbuzi wa muda mfupi tu: Kila jua likiwaka, greda inakuja kukwangua. Baada ya mvua mbili hali inarudi ile.

Tunaiomba Halmashauri ya Kisarawe na TARURA wajaze vifusi vya kutosha, washinde vizuri, na watengeneze mitaro ya zege ili barabara idumu.

Wananchi tunateseka, hatuna uhakika wa kufika majumbani wakati wa mvua.
 
Wilaya zote zinazoizunguka Dar es Salaam, ngumu sana kuendelea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…