Viongozi kumi (10) Bora Tanzania

Viongozi kumi (10) Bora Tanzania

Abraham Lincolnn

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2018
Posts
2,754
Reaction score
4,975
Tanzania imebahatika kuwa moja ya nchi iliyopata kuwa na viongozi bora kabisa Afrika na hata duniani kwa ujumla.Viongozi hao wamepata kuwa na mchango mkubwa Tanzania na hata kwa bara la Africa. Tunaona mifano ya Mwl. Julius Kambarage Nyerere ambaye amepigania uhuru si kwa nchi ya Tanzania tu bali amekuwa na mchango mkubwa katika harakati za uhuru kwa nchi jirani kama Afrika Kusini, Zambia na Msumbiji.

Tanzania pia imepata kuwa na wanaharakati na wapigania uhuru mahiri walioweza kuitwaa nchi kutoka katika kucha za wakoloni. Tunaona wapigania uhuru na wanaharakati kama Kinjekitile Ngwale, Bwana Abushiri na Bibi Titi Mohammed. Viongozi kama Mtemi Isike, Chifu Mirambo, Mangi Meli na wengineo wengi ambao walikuwa viongozi wa kimila walikuwa mstari wa mbele katika mapambano ya uhuru na hatimaye kuikomboa na kutupatia Tanzania hii tunayoifurahia leo.

Bila kupoteza muda, Naomba niweke orodha fupi ya viongozi waliopata kuongoza Tanzania walioacha alama kubwa na historia ya kipekee kwa ubora wao na uwezo wao wa kiuongozi ambao pasi na shaka uliacha alama kubwa kwa watanzania.

Kwa sasa nitaweka orodha tu kwa kifupi ila nitarejea kuelezea kila mmoja kwa undani zaidi.Pamoja na kuongeza orodha mpaka kufikia kumi (10) Bora.

Updates; Moderators naomba mnibadilishie Title iwe Kumi (10) Bora badala ya Tatu (3) Bora. Ahsante

Viongozi Kumi (10) bora kuwahi kuwepo Tanzania.

1. Mwl.Julius Kambarage Nyerere (Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania)
images - 2021-04-14T194314.603.jpeg


2. Edward Moringe Sokoine ( Waziri Mkuu wa Tanzania 1977–1980 na 1983 - 1984)
JamiiForums-59270899.jpeg


3. John Pombe Magufuli (Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania)
images - 2021-04-14T194418.314.jpeg


4. Chief Mkwavinyika Munyigumba Mwamuyinga (Mkwawa) - Chifu wa kabila la Wahehe
Mkwawa.PNG



5. Benjamin William Mkapa (Rais wa Tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania)

images - 2021-04-14T194445.615.jpeg



6. Rashidi Mfaume Kawawa ( "Simba wa Vita" - Waziri mkuu wa Tanzania 1972 - 1977" )

kawawa.jpg



7.Ali Hassan Mwinyi ( Rais wa Pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1985 - 1995 )

Ali_Hassan_Mwinyi.jpg


8.Oscar Salathiel Kambona ( Waziri wa Mambo ya Nje 1963–1966 )

kambona.JPG


9. Jakaya Mrisho Kikwete ( Rais wa Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 2005 - 2015)

Jakaya_Kikwete_2011_(cropped).jpg


10. Abeid Amani Karume ( Rais wa kwanza wa Zanzibar 1964 - 1972 )

karume.jpg
 
Kiongozi mzuri kufuatana na ubora
1. Kajala Masanja ; ameiongoza familia yake vizuri ambayo ina paula Na majani
2. Harmonize: ameiongoza vema konde gang, mpaka imetrend
3. Paula majani: amekuwa kiongozi mzuri kwa wanafunzi wenzake kwa muda mrefu na ndani ya muda mfupi ametumia ujuzi wa uongozi kutrend east africa

N A W A S I LI S H A
 
Kwa mijibu wa... nani?

Labda huyo Mkwawa tu ila hao wengine mmh!
 
Kichwa cha habari kinasema Tatu bora ila wewe umeweka zaidi ya Watatu kwenye bandiko..

Hujapishana uongo sana na mmoja wapo alichowafanyia watanzania miaka yake kutawala..
IMG_20201028_173703.jpg
 
Mbona hukumuweka mzee Mwinyi ambae ametutoa katika hali ya kupiga mswaki na mkaa, kusimama juani kusubiri nusu kilo ya mchele tena mdundiko, kwenda harusini au kweny kasherehe na suruali iliyojaa viraka, chachacha kuwa ndio style ya viatu vya watoto wa mjini.

Nafikiri Mwinyi alistahili kuwa ktk list hii maana amefanya mengi ya maana ktk nchi hii, hata Mkapa kaja kakuta kila kitu kawekewa mezani na yeye akatelezea mle mle kama ganda la ndizi.

Kabla ya Mwinyi ilikuwa ukikutwa na dawa ya mswaki tu au sabuni ya kuogea basi asubuh mgambo wanakuja kuizunguka nyumba yako kwa kosa la kuhujumu uchumi wa nchi
 
Viongozi bora ambao hawakuwahi kuwa Marais

Oscar Kambona

Edward Sokoine

Salim Ahmed Salim

Mark Mwandosya
Kiongozi ni kiongozi mkuu.Hata akiwa diwani.Viongozi hususan wakuu kama mawaziri,waziri wakuu,Rais na viongozi wengine wakuu wanaonekana machoni pa wengi.Hivyo tusitenganishe Marais na Viongozi wengine.Pia hao wanaweza kuwepo mkuu, Ila sio 3 Bora au 5 Bora.Ngoja tuongeze List huenda wakawepo 10 Bora.

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom