Viongozi kupiga picha na makarani baada ya kuhesabiwa, je sio kupoteza muda Au walikuwa spesho kwa ajili yao tu?

Viongozi kupiga picha na makarani baada ya kuhesabiwa, je sio kupoteza muda Au walikuwa spesho kwa ajili yao tu?

Lanlady

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2019
Posts
1,836
Reaction score
6,303
Naomba kwa wenye fikra yakinifu zisizoegemea upande wowote, wanisaidie kujibu hili swali.
Maoni yawe ni baada ya kuhesabiwa na sio wakati zoezi likiendelea
 
Hizo picha wangejigawa ingependeza. Leo madam prezda, kesho makamu, then pm, spika

Wote kupiga siku moja inaleta sintofahamu kwa wananchi wa kawaida
 
mhh kwa upande mmoja unaweza sema wanawatia wananchi hamasa. tuangalie hizo siku walizopewa watafanikisha jambo kwa asilimia ngapi
 
Kwahio leo watu wamebaki majumbani kuwaangalia viongozi ili wahamasike ?
Sasa huo ni mtazamo wako mkuu, sababu sijasikia mtu yoyote akisema tuwashe tv tuwaangalie viongozi
 
mhh kwa upande mmoja unaweza sema wanawatia wananchi hamasa. tuangalie hizo siku walizopewa watafanikisha jambo kwa asilimia ngapi
Sina tatizo na waliopiga wakati zoezi linaendelea. Ila kwa wale waliopiga baada ya zoezi kukamilika.
Mfano hawa hapa,👉👉👇
 
Attachments

  • Screenshot_20220823-183812_1.jpg
    Screenshot_20220823-183812_1.jpg
    39.2 KB · Views: 5
  • Screenshot_20220823-184106_1.jpg
    Screenshot_20220823-184106_1.jpg
    78.3 KB · Views: 5
  • Screenshot_20220823-184138_1.jpg
    Screenshot_20220823-184138_1.jpg
    46.5 KB · Views: 4
Wangeanza na walipa kodi+tozo kwanza

Ova
 
Maendeleo ya teknolojia yanatumika kwa uhamasishaji.
 
Nimeacha kazi zangu kusubiri kuhesabiwa hadi saa 6 hawajafika alafu nimeona mkuu wa wilaya mmoja anapiga picha na kunywa kahawa na makarani kama 6 kwahiyo mimi nisubiri Hadi amalize kutengeneza Kiki ndo nije kuhesabiwa? Kwanini hizo picha asingepiga nao jana Kama anawependa sana? Sasa sitaki kuhesabiwa
 
Nyie makarani mkifika huku nlipo kweli ntawaona nyie ngoma ngumu
Na kweli mmedhamiria kuhesabu
Watu sensa...

Ova
IMG-20220719-WA0024.jpg
 
Ni njia mojawapo ya kuhamasisha wananchi.
Wameonyesha mfano halisi

Hao viongozi wana ushawishi gani mpaka watumike kama mfano halisi? Maana kama kweli ni zoezi serious la kuhesabu watu, iweje lichague viongozi mbele mbele?
 
Hao viongozi wana ushawishi gani mpaka watumike kama mfano halisi? Maana kama kweli ni zoezi serious la kuhesabu watu, iweje lichague viongozi mbele mbele?
Mbona wananchi nao wamehesabiwa baadhi
 
Back
Top Bottom