Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Hamasa miongoni mwa nchi za kiislamu kuhusu vita vinavyoendelea Gaza zimepanda zaidi.
Viongozi watatu ndio waliozungumza kwa hasira kwenye mkutano wa mazingira unaoendelea huko Dubai.
Raisi Erdogan amesema vita vikimalizika Benjamin Netanyahu itabidi ashtakiwe kwenye mahakama ya uhalifu wa kivita.
Kiongozi wa Jordan mfalme Abdalla yeye akataka Umoja wa mataifa uilazimieshe Israel kusitisha vita huko Gaza.
Emir wa Qattar, Tamim althani akasema ni aibu kubwa kwa ulimwengu kuacha vita viendelee kwa ukatili namna hii huko Gaza.
Viongozi wote watatu tunaweza kusema wamezungumza utumbo na upuuzi wa hali ya juu. Afadhali wangenyamaza tu wakaficha ujinga wao.
Tuanze na Erdogan.Kwanini anasubiri vita viishe na ushindi uende kwa Benjamin Netanyahu.Kwani akishtakiwa kwenye mahakama ya uhalifu wa kivita ndio itakuwa nini na jee hata akihukumiwa kifo jambo ambalo si rahisi.
Je, kifo chake hicho yeye mmoja itakuwa ni sawa na kuipoteza Gaza au ni sawa na vifo vya watu zaidi ya 20000 na hasara ya tillion za dola.Jee yeye muda huu hana msaada mwengine wa kuzuia vita zaidi ya mdomo wake na utabiri wa bundi.
Emir wa Qattar ni moja ya watawala wa mashariki ya kati ambao wana mchango mkubwa kwa maslahi ya wapalestina na ana huruma sana juu yao. Hata hivyo yeye hakupaswa kuwa na maoni kama ya kwangu mimi.Kwanza nchini kwake kuna vituo vikubwa vya jeshi la Marekani ambavyo mara kadhaa vimetumika kupiga nchi za waislamu wenzake kama vile Afghanistan, Iraq na Libya. Angepaswa kama amekasirika avifunge kabisa.Na kama maumivi yake ni makubwa akiona watoto na raia wanauliwa na kunyimwa chakula basi na arushe ndege zake za kisasa akapige ndani ya Israel au apige maslahi ya Israel na Marekani ambayo yamemzunguka kila upande.
Mfalme Abdalla wa Jordan naye anataka umoja wa mataifa uilazimishe Israel isitishe vita.Kwani yeye hajui kuwa Israel ina maazimio zaidi ya 200 kuhusu Palestina na yote imeyapuuza.Kutakuwa na kitu gani kipya cha kuilazimisha kutekeleza agizo hilo jipya.
Yeye akiwa ndio jirani wa karibu zaidi na Israel anashindwa nini kuachia vijana wake kwenda kuokoa mashamba na majumba ya wapalestina yanayovunjwa na kuporwa na wazayuni sambamba na kufukuzwa kwenye mashamba yao.