Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Kero ni ile hali ya maudhi madogo madogo na mara nyingi kwa mtu binafsi au kikundi kidogo tu cha watu. Mfano wa kero inaweza kuwa jirani yako anayefungulia mziki mkubwa unaoleta usambufu kwa majirani wengine, mlevi anayetukana hovyo mtaani, kuachwa na mume bila kupewa mali stahiki, mwenyekiti wa mtaa anayekusanya pesa za takataka lakini takataka hazizolewi na mambo mengine yanayofanana na haya. Kero mara nyingi sio mambo ya umma bali binafsi au yatu wachache tu.
Matatizo ni shida na hasa zile kubwa na zinazoathiri sehemu kubwa ya watu na kwa muda mrefu mfano ukosefu wa maji, barabara mbovu, umeme kukatika, njaa kwa jamii, ukosefu wa usalama na mambo mengine kama haya. Matatizo ni jambo linalohitaji nguvu kubwa zaidi. Matatizo mara nyingi ni mambo ambayo hihitaji kuambiwa bali yanaonekana tu muda wote.
Sasa viongozi wa CCM wa serikali na chama katika misheni zao wanasikiliza na kutatua kero au matatizo ya raia?