Viongozi wa CCM na kauli kinzani kwenye suala la utekaji, wananchi wabebe lipi?

Viongozi wa CCM na kauli kinzani kwenye suala la utekaji, wananchi wabebe lipi?

Rabbon

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2022
Posts
21,625
Reaction score
33,688
Salaam, Shalom!

Sintofahamu inaendelea katika vyama vya siasa, wakati huu ni chama cha kijani.

Katibu Mkuu wa chama cha kijani ametoka mbele na kukubali kukaa meza moja na kupata picha ya pamoja na katibu mkuu mwenzie wa chama cha bluu, akaenda mbali zaidi kwa kukemea mauaji ya wananchi yanayofanyika na wasiojulikana, kisha akaagiza vyombo vikomeshe hali hiyo, kwa mbali niliona pressure ya wananchi ikishuka na tabasamu KUREJEA.

Upande wa pili, Mwenyekiti wa chama cha kijani, anatoka kuuambia umma kuwa kifo ni kifo tu, kwamba wananchi wasihamaki ilhali kifo hicho kimetokana na mauaji tena ya mtu kutekwa hadharani na kufungwa pingu kisha kwenda kuuwawa🤔

Sasa swali linakuja,

Je, kati ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu wa Chama cha Kijani, wananchi wamuelewe nani?

MUNGU ibariki nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿.

Karibuni🙏
 
Hapo hapo anadai aliapa kuwalinda wananchi kuhakikisha Amani inatawala Kisha anadai kifo ni kifo tu,

Mtu atekwe, apigwe pingu hadharani, akauwawe Kisha aseme kifo ni kifo!!
 
Mwenyekiti wetu na Katibu mkuu wetu wameeleweka vyema sana kwa watanzania.ndio maana wameungwa mkono vyema sana.acheni kuleta uchochezi.acheni vyombo vya dola vifanye uchunguzi wa kina na kuleta ripoti kamili
Ni wapi mkt ameonyesha kuhuzunishwa na tukio la mtu KUPIGWA pingu ndani ya bus Kisha kwenda kuuwawa na mwili wake kutupwa?

Kwa maoni yangu, katibu mkuu wa chama Cha kijani, ameeleweka vilivyo na wananchi kuliko Mwenyekiti.

Wewe unaonaje Lucas?
 
Mwenyekiti na Katibu Mkuu wako sahihi kabisa tatizo ni Chadema Wanataka kulifanya swala la Kifo Cha Shujaa Ally Mohamed Kibao kuwa la kisiasa Zaidi na Kiislam 🐼
Jibu swali Jo!!

Kati ya Mwenyekiti wa kijani na katibu wa kijani, nani Hasa ameeleweka Kwa umma wa wananchi?

CHADEMA haijadiliwi hapa, hiki ni kikao Cha ndani!!
 
Mwenyekiti ni 🚮...period
Yaani uwaambie polisi kifo ni kifo, hivi watachunguza Kweli kifo hicho Kwa kauli hiyo?

Nadhani Katibu mkuu wa kijani ameupiga mwingi sana kuliko mkt wake.
 
Back
Top Bottom