Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 15,692
- 23,038
Zile kauli za kwamba "wameichezea sana hii nchi", au "wametunyonya sana" au ziwe ni historia.
Mabeberu wote wana tabia kubwa moja, nongwa.
Ukisema kitu kimoja hadharani wao wanakirekodi na kukiweka ili kije kuwa ni kumbukumbu juu yako wewe mwenyewe.
Hivyo jitihada zote za serikali ya awamu ya tano, kujenga madaraja, SGR, ununuzi wa ndege na miradi yote mikubwa ya maendeleo, zifanyike kimyakimya.
Mpaka sasa serikali naipa alama ya 5/10 kwa kukaa kimya juu ya yanayoendelea.
Cha msingi ni kwamba serikali haina jinsi ila kusikiliza kila upande na kuchambua kipi cha kujibu na kipi cha kukipuuza.
Uchaguzi wa 2020 ndo utakuwa wa kusuka au kunyoa na endapo CCM itashinda uchaguzi huo basi yajayo hayatabiriki.
Upinzani unaweza kushinda lakini endapo tu wananchi wataamua hivyo na si vinginevyo.
Ila kwa sasa serikali iwe makini na namna inavyojibu taarifa au matamko kutoka kwa mabeberu.
Namshauri waziri Kabudi na macho yake yale makubwa awe mwangalifu sana maana huonyesha hamaki khasa anapowaongelea hawa watu.
Na jambo la busara ni kukaa kimya na kuyashughulikia badala ya kukurupuka kujibu.
Weekend njema.