Viongozi wa CCM na serikali waziwazodoe na kuwasema mabeberu. CCM ikishinda tena uchaguzi wa 2020 ifanye mambo yake kimyakimya.

Viongozi wa CCM na serikali waziwazodoe na kuwasema mabeberu. CCM ikishinda tena uchaguzi wa 2020 ifanye mambo yake kimyakimya.

Richard

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2006
Posts
15,692
Reaction score
23,038
Zile kauli za kwamba "wameichezea sana hii nchi", au "wametunyonya sana" au ziwe ni historia.

Mabeberu wote wana tabia kubwa moja, nongwa.

Ukisema kitu kimoja hadharani wao wanakirekodi na kukiweka ili kije kuwa ni kumbukumbu juu yako wewe mwenyewe.

Hivyo jitihada zote za serikali ya awamu ya tano, kujenga madaraja, SGR, ununuzi wa ndege na miradi yote mikubwa ya maendeleo, zifanyike kimyakimya.

Mpaka sasa serikali naipa alama ya 5/10 kwa kukaa kimya juu ya yanayoendelea.

Cha msingi ni kwamba serikali haina jinsi ila kusikiliza kila upande na kuchambua kipi cha kujibu na kipi cha kukipuuza.

Uchaguzi wa 2020 ndo utakuwa wa kusuka au kunyoa na endapo CCM itashinda uchaguzi huo basi yajayo hayatabiriki.

Upinzani unaweza kushinda lakini endapo tu wananchi wataamua hivyo na si vinginevyo.

Ila kwa sasa serikali iwe makini na namna inavyojibu taarifa au matamko kutoka kwa mabeberu.

Namshauri waziri Kabudi na macho yake yale makubwa awe mwangalifu sana maana huonyesha hamaki khasa anapowaongelea hawa watu.

Na jambo la busara ni kukaa kimya na kuyashughulikia badala ya kukurupuka kujibu.

Weekend njema.
 
Mbuzi anaetaka kupandwa na beberu sikuzote lazima awe na makeke mengi hiyo ni nature na huwezi pingana nayo
 
Cha msingi ni kuhakikisha kunakuwepo uwiano sawa kati ya "give" na "take" kati ya wanyonge na mabeberu.
 
Ungewajua wazungu walivyo na jinsi wanavyo waza juu yako sokwe usinge kuwa unasema mambo kama hayo. Wewe kwao ni sokwe tu hata ukijipendekeza namna gani utabaki kuwa sokwe tu kwao. Wazungu wamaheshimu rangi yao.

Nimesikiliza idhaa moja ya ulaya leo, sitaki kuitaja jina, kwao walikuwa wakizungumzia ugonjwa wa corona virus.
Wanasema kama huu ugonjwa ungekuwa Afraka ingekuwaje? Alafu wakaonyesha jinsi watu wanavyo ishi Bush bila hospitali na huduma nyingine, wakati wanajua fika kuwa Afrika ins miji mikubwa na majengo mazuri tena mengine kuliko hata kwao, viwanja vya ndege na kadhalika, lakini wao wanajitahidi kutoa picha ya kwamba sisi ni holes, hatuwezi survive bila wao.

Kwa hali hiyo sishangahi kama wakoma kama nyie mnakuwa na tabia za kubeza serikali zenu. Mnafikiri nyie ni nani kwanza kwao?
Muwapende msiwapende kwao ni sawa tu. Nyie ni masokwe!!!
 
Unawezaje kumficha mhisani wako wkt ukifulia unaenda kugongea kwake big time. Hlf lazma tujinadi mtajuaje maendeleo tuliyoyafanya wkt ndo silaha yetu kubwa??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ungewajua wazungu walivyo na jinsi wanavyo waza juu yako sokwe usinge kuwa unasema mambo kama hayo. Wewe kwao ni sokwe tu hata ukijipendekeza namna gani utabaki kuwa sokwe tu kwao. Wazungu wamaheshimu rangi yao.

Nimesikiliza idhaa moja ya ulaya leo, sitaki kuitaja jina, kwao walikuwa wakizungumzia ugonjwa wa corona virus.
Wanasema kama huu ugonjwa ungekuwa Afraka ingekuwaje? Alafu wakaonyesha jinsi watu wanavyo ishi Bush bila hospitali na huduma nyingine, wakati wanajua fika kuwa Afrika ins miji mikubwa na majengo mazuri tena mengine kuliko hata kwao, viwanja vya ndege na kadhalika, lakini wao wanajitahidi kutoa picha ya kwamba sisi ni holes, hatuwezi survive bila wao.

Kwa hali hiyo sishangahi kama wakoma kama nyie mnakuwa na tabia za kubeza serikali zenu. Mnafikiri nyie ni nani kwanza kwao?
Muwapende msiwapende kwao ni sawa tu. Nyie ni masokwe!!!

Sent using Jamii Forums mobile app

Wewe kweli ni sokwe uliezeeka yaani umeshindwa kabisa kuelewa nilichoandika?
 
Back
Top Bottom