Chagu wa Malunde
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 8,734
- 5,750
Hii ni dalili kuwa hamlitakii mema taifa letu na ipo siku mtaliletea janga kubwa. Ndio maana aliyekuwa mbunge wa Temeke kupitia CCM aliwahi kutoa ombi kuwa Chadema ni chama cha wapenda vurugu hivyo kinastahili kufutwa.
Baada ya kushindwa uchaguzi kwenye box la kura na wananchi kuichagua Ccm sasa mnataka kuiaminisha jumuia ya kimataifa kuwa hapa Tanzania kuna ukiukwaji wa haki za binadamu. Je mbona mlipokuwa wabunge hizi propaganda zenu hatukuzisikia?
Sasa hivi mmezua mchezo mchafu eti mnatafuta hifadhi kama wakimbizi wa kisiasa kuwa kuna tishio la kuuliwa na vyombo vya dola. Mnachotaka tu ni kuchafua taswira ya nchi yetu kuwa hakuna amani na kuna ukiukwaji wa haki za binadamu. Je kama kuna ukiukwaji wa haki za binadamu mbona UN wapo kimya na wana ofisi hapa Tanzania.
Kama vyombo vya dola vilitaka kumuua G Lema wangemuacha yupo salama wiki zote hizi mbili tangu uchaguzi uishe? L Nyalandu anatafuta kick kuwa anakimbia kuuliwa hivi mwanasiasa ambae unataka kuuliwa watu watakuacha hizi siku zote upo salama?
Godbless Lema alipokuwa mbunge alikumbana na kesi nyingi sana,na mpaka alikaa mahabusu miezi minne mbona alipotoka mahabusu hakukimbilia Kenya kwenda kuomba hifadhi kama mkimbizi wa kisiasa?
Kwa ujumla ni kutokubali matokeo ndio sababu ya kutaka kuchafua taswira ya nchi yetu. Na kukosa ubunge ambao kwenu mlidhania nia ajira za kudumu ndio sababu mnataka kwenda kujifanya wakimbizi.
Na hii propaganda mlioamua kuitumia itabuma na mtaaibika zaidi na huu ndio unaenda kuwa mwisho wenu mbaya kisiasa. Maana watanzania wana akili na hawadanganywi kitoto.
Nota bene : Kila propaganda mlizoanzisha zote zilibuma,kumbukeni wakati wa Covid-19 mlipata aibu kubwa,amabayo imewanyima kura.