Mleta mada ana uwendawazimu fulani. Waliosema vile hawakumaanisha kuwa hawataki usafiri wa ndege. Siyo lazima usafiri wa ndege utolewe na serikali.
Nafikiri ikitokea siku serikali ikaamua kuanza kujenga restaurants kila kijiji, watu wakasema siyo kipaumbele, halafu serikali ikajenga na kisha kuzifunga restaurants zote za watu binafsi, siku waliosema ujenzi wa restaurants kwa serikali siyo kipaumbele, wakaonekana wanakula kwenye hizo restaurants, kuna wapumbavu watawapiga picha na kusema kuwa kwa nini wanakula chakula kwenye restaurants ambazo walisema siyo kipaumbele cha serikali?
Tuna watu wendawazimu wengi. Mtu kusema kitu fulani siyo kipaumbele cha serikali haimaanishi kuwa kitu hicho siyo muhimu kwa maisha yake.
Serikali hata isiponunua ndege, watu bado watapande ndege. Jambo baya lililofanyika ni kuiua Fastjet iliyokuwa inatoza nauli ndogo ili kuwalazimisha watu wote watumie ATCL.
Kuna huduma ambazo serikali isipozitoa, hakuna atakayezitoa japo huduma hizo ni muhimu sana kwa binadamu.