Shalom. Naomba VIONGOZI wa CHADEMA Mh Heche rudisheni panga alani mrudi mjipange. Mkakati niuonao rohoni sio mzuri la sivyo manakwenda kuzima taa ya ukombozi wa Watanzania.
Nionavyo barua ya msajiri msiichukulie poa. Kinachoundwa ni kuwatengua viongozi wote wakuu rejea barua ya msajiri. Kisha watamdaka Heche na kumuweka ndani kinachobaki ni umbwe la uongozi kisha Mwenyekiti mstaafu atarudi na hawa waliojiuzuru watakaa fasta na kufanya uchaguzi kama wana CHADEMA na uongozi mpya kuingia mkija toka kifungoni ( uongozi wa sasa) hamatakuwa na chenu mtabakia kukimbilia nje ya nchi kitu ambacho mtaruhusiwa kufanya biashara inakuwa imekwisha nchi inaingia kizani tena.
Ushauri wangu sitisheni mikutano yote inatosha kwa sasa kwani imeonesha mnaungwa mkono na Watanzania wengi. Rudini mezani mjaze kwa haraka nafasi zilizoachwa wazi na waliojiuzuru muunde kamati kuu kwa mujibu wa katiba. Rudini mjipange kukabiliana na barua ya msajiri na ile kesi iliyofunguliwa. Naomba tafadhari msitishe mikutano maana itapelekea kukamatwa kwa viongozi zaidi.
Pia naomba muache kutuo lugha zisizo za staha kwa polisi nimefutilia mkutano wa Igoma ikizingatia sio polisi wote ni wabaya na mkizingatia hiyo ni ajira inayolisha familia zao na ni kazi ya kiapo cha utii ni sawa na mtu akuambie usifanye siasa.