nguruka wa kig0ma
JF-Expert Member
- Jan 16, 2020
- 2,943
- 2,935
Hili siyo sawa,hukumu tu imetosha kuwapa umaarufu ndani na nje ya Tz. Nawashauri viongozi waliobaki gerezani wasithubutu kupokea msamaha toka kwa Jiwe,watampandisha chati isivyo kawaida.Wanajamvi,
Baada ya kumuona ndugu Polepole akikenua meno baada ya kumlipia Dr Mashinji milioni 30 na kutoka gerezani, nimeona kama vile hii hukumu kuna kamchezo fulani hivi kalichezwa ambako kana ukakasi hasa ukizingatia umuhimu wa uhuru wa mahakama pamoja na haki za kisheria za viongozi hao walioswekwa ndani. Inafahamika wazi kuwa polisi ndiyo waliomuuwa Akwilina.
Natambuwa jitihada zinazoendelea za michango ya kuwalipia. Lakini kama ni kweli kuna wafungwa wengi ambao wako ndani kwasababu za kisiasa na ambao wameshindwa kulipa pesa, kuwalipia hawa viongozi peke yao itakuwa ni usaliti, na hivyo nashauri viongozi hao wa chadema wasalie ndani magereza hadi hapo watakapoachiwa bila masharti na haki kutendeka kwa wote waliofungwa kwa kubambikiziwa kesi na sababu za kisiasa. Ni wakati pia wa kudai haki kwa wale ambao hawajapatiwa haki zao kwa kuuwawa, kutekwa, kushambuliwa, kufungwa jela nk.
Suala kubwa liko kwenye pesa ambazo zimeshachangishwa. Hilo ni suala linaloweza kufanyiwa kazi kwa maoni kutoka kwa wachangiaji hao pamoja na viongozi wa chadema.
Kwa maoni yangu, kadri viongozi wa chadema wnavyozidi kukaa gerezani, ndivyo ambavyo umaarufu wa ccm ndani na nje ya nchi unadidimia. Ushauri wangu kwa ccm, muwaachie huru viongozi wa chadema waendelee kutoa hoja zao kwa wananchi kwa uhuru kama katiba inavyosema. Na tume huru ni LAZIMA.
Kwasababu kutokana na kauli ya wamarekani kwamba kesi hii ni unyanyasaji dhidi ya wapinzani, ina maana kwamba viongozi wa chadema walioko gerezani, wanachukuliwa kuwa ni wafungwa wa kisiasa na wala siyo wahalifu kama ccm inavyotaka waonekane mbele za macho ya wapiga kura.
View attachment 1384360
.
Sent using Jamii Forums mobile app