Viongozi wa dini nawasihi kuandaa siku maalum kuliombea taifa.

Viongozi wa dini nawasihi kuandaa siku maalum kuliombea taifa.

Isalu

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2022
Posts
504
Reaction score
665
Naomba kuwasihi viongozi wote wa dini nchi Tanzania kuandaa siku maalum kuliombea taifa na kuwashtaki kwa Mungu wahusika wote kwenye ubinafsishaji huu utakaolitumbukiza taifa shimoni hadi vizazi vijavyo.

Kwa waislam zisomwe albadir na kwa wakristo zigongwe kengele mara3 kuashiria msiba na maombolezo dhidi ya yeyote aliyehusika kupitisha huu mkataba utakaoleta mateso kwa taifa huku wachache wakineemeka na familia zao.

Ardhi ifungue kinywa iwameze wote. Ee Mwenyezi Mungu tunakuomba na kukusihi, kwa kuwa Jina lako ni takatifu na la kuogopwa. Nchi hii umetupa wewe Mungu. Nyoosha mkono wako uliokoe taifa lako.

Amen.
 
... maombi yaongozwe na Kadinali, Malasusa, na Alhadi? Yupo wa kusema kwa kumaanisha nendeni mkamwambie mbweha yule? Au "watamwombea mbweha"? Sijui.
 
Back
Top Bottom