Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ni mawazo yangu tu haya lakini.
Wenzetu waislamu nafikiri wanakuwa wanachanganya mambo fulani, mfano nafikiri kabisa wenda wanakuwa na mawazo kwamba islamu duniani kote ni rukusa na lkinyume chake si ruksa.
Mfano utakuta wanaandamana sana ku force kujenga na kuendeleza tamaduni za kiislamu sehemu ambayo si ya kiislamu, lakini ukijarabu kuishi kwa tamaduni zako ktk dunia ya islamu wana kuchinja ama kukuchapa viboko.
Mfano kuna wazungu fulani sikumbuki ktk nchi gani ya kiaarabu kama sikosei ilikuwa Saudia arabia walikuwa wamevaa bukta wakakumbatiana ktk haraiki na kupeana busu ,Hawa jamaa waliwakamata hawa wazungu kuwachapa viboko na kuwarudisha, Wakati kwa wazungu swala la kumpa busu mwezio ndo unaonekana una maadili.
Sasa angalia Ubelgiji wao wanalazimisha kuvaa mavazi ambayo siyo maadili kwa wabelgiji, wakiambiwa wanakuja juu. Wenzetu lazima nafikiri wakubali kwamba vazi unaloona kwako ni la maadili kwa mwenzio sio la maadili vilevile, kwa hiyo angalau wangekuwa na fair fulani ktk maadili mfano na wao huko ktk dunia ya islamu ivumilie tamaduni na maadili ya wengine.
Swala la mavazi huwezi sema hili ni vazi la maadili ,kwani linategemeana na mazingira, mfano huwezi sema mwanamke wa kiafrika avae gauni, sketi ama kitenge nchini urusi MOSCOW, mama huyu atakufa tu kwa baridi ni lazima agande. Ndivyo hivyo nafikiri mavazi ya islamu ni tamaduni ya waarabu kuishi jangwani ambako kuna upepo mkali na mchenge mwepesi ambalo linasababisha vumbi kali.Hivyo yale mavazi ni mavazi staili ktk mazingira ya waarabu kule jangwani na sio kwa mazingira kama DAR.
Mavazi yale bado nafikiri hayakutengenezwa kwa ajili ya kuwaficha wanawake zidi ya wanaume bali zidi ya upepo mkali na mchanga unaopiga masikio. Na ndio maana hata wanaume wanavaa vilemba wakiziba masikio. cha kujiuliza kwani wanaume wanaziba masikio kwa sababu masikio ya wanaume ni kivutio na matamanisho kwa wanawake.? jibu ni hapana.
Hakuna part, ya mwanadamu ambayo ni tamanio dhidi ya mwezake hilo ndo jibu sahihi, ila kutamani ni kwa sababu mtu husika unaamuwa kuiambia roho yako mtamani fulani. Kwani mnataka kutuambia ya kwamba babu zetu waliokuwa wanavaa makuti kuziba sehemu za mbele tu walikuwa wanatamaniana kila sekunde? ama walikuwa hawana maadili kwa kuvaa makuti?
Ndivyo vivyo hakuna Program ambayo inaweza kukusababisha ukose maadili, ila ni mhusika tu mkosa maadili anakuwa amekosa maadili toka akiwa tumboni mwa mama yake.
Ndio maana angola wameifuta
the laws of allah
ukafiri una nguvu lakini hauwezi kushindana na mungu
wanao uhuru wa kuwakataza au kuwaonya waumini wao wasiangalia Dstv, lakini sidhani kama wanao uwezo kisheria 'kuban' Dstv isionyeshwe eneo hilo kwani leseni ni kwa ajili ya nchi nzima.
Waafrika bado tuna tatizo na haki za binadamu, maana hawa masheikh na hata wachungaji na mapadri wana tabia za kupenda kushawishi mambo ambayo kwa kweli yanaendana kinyume na uhuru wa binadamu. Mfano si ajabu kusikia ukiwa Dar kwenye misikiti na mahubiri hawa watu wakiwadhalilisha wanasiasa ambao imani zao ni tofauti na za kwao.
Ndio maana mi nimeamua kuachana na hizi dini zote hadi hapo nabii wa kweli wa kiafrika atakapokuja, ama sivo nitaendelea kuwa agnostic, no point...
weza
Nakuunga mkono mkuu,umezungumza kitu cha maana. Kinachotakiwa ni serikali ya Kenya kukutana na viongozi wa kiislam na DSTV kutatua tatizo hilo.
Maadili according to who? Wanakomalia mavazi kisha wanafuga mapepo, kuua binadamu wasio na hatia kwa ugaidi na kugombania sadaka misikitini!
Dini zingine ni laana za Dunia