Viongozi wa dini ya Kikristo wanazidi kuwindwa, wengine wameshakimbia nchi, SHIDA NI NINI??

Viongozi wa dini ya Kikristo wanazidi kuwindwa, wengine wameshakimbia nchi, SHIDA NI NINI??

Wote wa dini ile wanamkubali malkia?

  • Ndio wote tunamkubali

    Votes: 1 7.1%
  • Hapana hata sisi hatumkubali

    Votes: 13 92.9%

  • Total voters
    14
Mayor Quimby na Kiranga wame sema sana humu kuwa watanzania wengi hamjui kuchambua mambo kwa uhalisia, mna endeshwa na hisia plus mihemuko ya mawazo yenu.

suala la mauaji yana fanyika kila siku, hawajali wewe ni mkristu, muislam au mpagani as long as uko kinyume na wao basi hauko safe kabisa.

Badala ya kukemea mauaji, mme anza kujigawa kwa kuitisha attendence ya kidini eti hawa waislam hawa wakristu.

tukisema na haya maandamano yagawiwe kwa dini, kutakuwa na lolote la maana ki nchi?.
Kwahiyo hao uliowataja WAKISHASEMA inatakiwa wote tutoe maoni KULINGANA NA MAWAZO YAO? kila mtu si ana uhuru wa kutoa maoni kulingana na mawazo yake? Kama unajiona tunajigawa sawa, nawewe pambana bila kujigawa.
 
Wabongo wengi ni wadini sana.

Wanauawa na kutekwa watu wa dini zote, lakini sasa suala lishafanywa la kidini.

Dini zenyewe ujinga mtupu.
Muda mwingine nakubaliana na wewe kuwa logical thinking yetu bado sana, yaani full kuendeshwa kwa mkumbo na hisia ziziso weza kuchambua kwa hoja.

Kuna vijana wengi wa kimasikini wana kamuliwa na kupotezwa daily, sidhani kama mtoa mada na great thinker's wenzie kwenye huu uzi wana attendence ya kujua majina yao sembuse dini zao.

Tuna rudi hatua mia nyuma, mapambano si dhidi ya udhalimu uliopo bali ya imbalance ya mauaji ya wana dini.
 
Kwahiyo hao uliowataja WAKISHASEMA inatakiwa wote tutoe maoni KULINGANA NA MAWAZO YAO? kila mtu si ana uhuru wa kutoa maoni kulingana na mawazo yake? Kama unajiona tunajigawa sawa, nawewe pambana bila kujigawa.
Una eleweshwa kwa hoja, sijasema mawazo yao ni sahihi kwamba hawa kosei ila most of the time wana sema ukweli juu ya hili au lile.

wewe una hisia za kutaka mjadala uwe wa kidini, bila ya kuwaza effects ya hiki unacho kichochea hapa.
 
Muda mwingine nakubaliana na wewe kuwa logical thinking yetu bado sana, yaani full kuendeshwa kwa mkumbo na hisia ziziso weza kuchambua kwa hoja.

Kuna vijana wengi wa kimasikini wana kamuliwa na kupotezwa daily, sidhani kama mtoa mada na great thinker's wenzie kwenye huu uzi wana attendence ya kujua majina yao sembuse dini zao.

Tuna rudi hatua mia nyuma, mapambano si dhidi ya udhalimu uliopo bali ya imbalance ya mauaji ya wana dini.
Wabongo wanataka kufanya maandamano kuing'oa CCM lakini wameshindwa kufanya bank run kuigomea CRDB ilivyowahanithi pesa zao wenyewe.

Hii nchi ina vituko sana.
 
Tunavyokabiliana na hizi nguvu za giza zilizoshika nchi ya Tanzania na dunia kwa ujumla, tusisahau ilitabiriwa kuwa siku za mwisho kuelekea kurudi kwa YESU watu wa MUNGU watapitia dhiki nyingi.

Tunasubiri mpinga Kristo afunuliwe dhiki kuu ianze..

"Kisha huyo mnyama akaruhusiwa kusema maneno ya kujigamba na kumkufuru Mungu; akaruhusiwa kuwa na mamlaka kwa muda wa miezi arubaini na miwili.

Basi, akaanza kumtukana Mungu, kulitukana jina lake, makao yake, na wote wakaao mbinguni.

Aliruhusiwa kuwapiga vita na kuwashinda watu wa Mungu. Alipewa mamlaka juu ya watu wa kila kabila, ukoo, lugha na taifa.

Wote waishio duniani watamwabudu isipokuwa tu wale ambao majina yao yameandikwa tangu mwanzo wa ulimwengu katika kitabu cha uhai cha Mwanakondoo aliyechinjwa.

Aliye na masikio, na asikie!

Aliyepangiwa kuchukuliwa mateka lazima atatekwa; wa kuuawa kwa upanga atauawa kwa upanga. Hivyo, watu wa Mungu na wawe na uvumilivu na imani."

Ufunuo.13.5-10.BHN


Dhiki kuu bado haijaanza, hizi ni rasha rasha, lakini kwakweli imekaribia.

I was listening to Dr. Christian the other day:


View: https://youtu.be/CK2-ct6p_xE?si=y4XPMx_Pwy9MSb_q


There is something going on on earth, sio tu Tanzania, duniani. Anayefikiri mambo yapo kama yalivyokuwa yuko kwenye usingizi mzito.

Either uamke au endelea kudhihaki.

Itakuwa kama ilivyokuwa siku za Noah. Kama siku za Loti.


"Mwana wa Adamu atakaporudi, itakuwa kama ilivyokuwa Nuhu alipoishi.

Watu walikuwa wakila, wakinywa, wakioa na kuolewa hata siku Nuhu alipoingia katika safina. Ndipo gharika ilikuja na kuwaangamiza wote.

Ilikuwa vivyo hivyo katika wakati wa Lutu, Mungu alipoteketeza Sodoma. Watu wa Sodoma walikuwa wakila, wakinywa, wakinunua, wakiuza, wakipanda na kujijengea nyumba.

Lakini siku ambayo Lutu alitoka Sodoma, moto na baruti vilinyesha kutoka mbinguni na kuwaua wote.

Hivi ndivyo itakavyokuwa siku ambayo Mwana wa Adamu atarudi."

luka.17.26-30.TKU


"Maana wakati huo kutakuwa na dhiki ambayo haijatokea tangu Mungu alipoumba ulimwengu mpaka leo, wala haitatokea tena.

Kama Bwana asingepunguza siku hizo hakuna binadamu ambaye angeokolewa. Lakini kwa ajili ya wateule wake, Bwana amezipunguza siku hizo.

“Basi, siku hizo, baada ya dhiki hiyo, jua litatiwa giza na mwezi hautaangaza.

Nyota zitaanguka kutoka angani, na nguvu za mbingu zitatikiswa.

Hapo watamwona Mwana wa Mtu akija katika mawingu kwa nguvu nyingi na utukufu.
"
Marko.13.19-26.BHN


Mimi binafsi nitatoka. Oktoba 29 ninatoka.

Lakini tusisahau unabii. Napata wakati mgumu ku reconcile baadhi ya hawa modern prophets na unabii wa kwenye biblia honestly..

They remind me of this:

"Manabii hao wanawapotosha watu wangu na kuwaambia ‘Kuna amani’, wakati hakuna amani. Watu wangu wanajenga ukuta usiofaa, nao wanaupaka chokaa!

Sasa waambie hao manabii wanaopaka chokaa ukuta huo kwamba itanyesha mvua kubwa ya mawe na dhoruba na ukuta huo utaanguka.

[16] mwisho wa manabii wa Israeli waliotabiri mema juu ya Yerusalemu na kuona maono ya amani hali hakuna amani. Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nimesema.
"
Ezekiel.13.10-16.BHN
 
Wawawe kiherehere wasidhani serikali ni wale mazombi wao wanaowalia sadaka
 
Back
Top Bottom