KERO Viongozi wa Kijiji cha Mlimba B, Halmashauri ya Mlimba, Wilaya ya Kilombero mkoani MOROGORO wananyanyasa wananchi

KERO Viongozi wa Kijiji cha Mlimba B, Halmashauri ya Mlimba, Wilaya ya Kilombero mkoani MOROGORO wananyanyasa wananchi

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Viongozi wa kijiji cha Mlimba 'B' katika Halmashauri ya Mlimba wamekuwa kero kwa wananchi kwani wamekuwa wakitoza faini ya Tsh. 10,000/= kwa kila mwananchi asipohudhuria kwenye mkutano wa serikali ya kijiji na kwenye shughuli za maendeleo ambazo ni kusafisha barabara ambazo zinafanyika kila siku ya Jumatano ya kila wiki.

Mbaya zaidi hizi faini zinatozwa kienyeji kiasi kwamba hakuna risiti wala uthibitisho wowote kuonesha mwananchi ametozwa faini hiyo.

Namna inayotumika kukamata ni migambo ambao wanaongozana na wajumbe wa serikali za mitaa ambao wanapita majumbani na kushika watu kama wezi. Wakifika wanakudai kiasi hicho cha pesa na kama huna unapelekwa ofisi ya kijiji ambapo unakutana na mtendaji wa kijiji, mwenyekiti wa kijiji na baadhi ya wajumbe wa Serikali ya kijiji kisha unaambiwa utoe 10,000/= hawatoi hata nafasi ujielezee wala hawataki kukusikiliza as long as umefikishwa kwao, unalazimika kutoa.

Pia kumekuwa na michango iliyokithiri ambayo tunaomba mamlaka husika zifuatilie kuona uhalali wa michango hiyo.
 
Poleni wana wa pakaya, ile road toka ifanyiwe feasibility kitambo sana aisee.
 
Sijawahi kuona serikali katili kama hii na kuongoza kwa malalamiko kutoka kwa wananchi bila utatuzi wwte. Poleni watanganyika Ila kunakitu kifanyike kujikomboa
Kazi ni kipimo cha utu
 
Viongozi wa vijijj wakiwa huko vijijini wanajikutaga hao🙌🙌🙌🙌🙌🙌
 
Kwahiyo usipolipa hiyo faini? Inakuwaje
kwakuwa hamjitambui na aagiza hiyo faini iwe elfu 30 na mikwaju ya kutosha
 
Back
Top Bottom