Hiyo Idadi ya Magari ya Mwalimu ni ya Mwaka Gani? Halafu wakati Mandela anakuja Tanzania Mwalimu hakuwa Rais wa nchi hii.
Halafu kusema watu wa Usalama wana Overrate hatari zilizopo ni kutokuwatendea haki. Misafara inaongozwa na Polisi na siyo watu wa Usalama.
Wengi wenu hamjui tu, kuongoza hiyo misafara ni polisi ndiyo wanaoteseka na kama wangekuwa na uwezo bila ya shaka, wangetaka hiyo misafara isitumie hata dakika tatu iwe imepita. Ukichunguza ni polisi ndiyo wanaoshinda mabarabarani kusubiri hiyo misafara ipite. Unadhani na wao wanapenda kukaa masaa kwa masaa kusubiri msafara upite?? Yaani Polisi wanafaidika na nini kuzuia watu kwa muda wote huo?
Kwenye hii picha Makamu wa Rais kasimamisha msafara wake kati kati ya barabara anahutubia. Kwa mazingira kama hayo Polisi wanaweza kuruhusu magari yaelekee alipo Makamu wa Rais??