Viongozi wa SADC wasalimu amri wa Kagame! Wakubali kuondoa vikosi vyao CONGO DRC. Huu ni ushindi kwa Kagame na hatari kwa mataifa yanayomzunguka

Kagame hana claim kwenye ardhi hiyo labda kama Mwami wa Rwanda angerejea kwenye throne Rwanda ndiye angeweza kudai ardhi ya iliyokuwa Kingdom of Rwanda kabda ya kunyang'anywa na Wakoloni wa kutoka Ulaya.
Hivi kuna sehemu yao kule?
 
Kivu ni himaya ya Ufalme wa Rwanda.
Ok... wale wabembe , wamushi wafulelo kwao wapi . Na theory ya mulenge as a refugee camp by 1959, and also the Belgian sending some people kule kuwa viongozi wa mashamba 1935 North Kivu. Na sehemu ya kaskazini mwa Urundi kuwa kongo ni famba.
 


Sasa Mama yetu na upolepole hivi hiyo reli inaenda wapi? Usalama badala ya kusaidia nchi wanashinda kumfuatilia Lissu. Yaani watu wanalipwa eti kufuatilia na hata kuteka wanasiasa wakati wenzetu wanapigania rasilimali na biashara huko Congo
 
Kagame kawatimua SADC huko Drc kwenye shamba lake.
 
Endeleeni kupelekeshwa na wanasiasa wakiskia Kuna maandamano
Jidanganye endelea kutumia jeshi letu kufanya usafi kisa maandamano ya chadema mtavuna mnachopanda JWZT kuingiza siasa ilikua kosa kubwa sana
 
14 March 2025
Kigali, Rwanda

MWANDISHI ALIYEFIKA MAENEO YANAYOKALIWA NA KUNDI LA M23 IKIWEMO GOMA, RUBAYA, MASISI N.K ASIMULIA NIDHAMU YA M23


View: https://m.youtube.com/watch?v=_1yxq9obOPs
Teddy Mazina anasema askari waasi wa M23 wana nidhamu ya hali ya juu, na ni watu wasomi waliotoka maeneo mbalimbali ya dunia walioamua kurudi makwao kama waKongomani wengine wa Mashariki mwa Kongo.

Na Kuwa M23 wamezingira kambi na airport ambazo ngome za kambi za SAMIDRC, MONUSCO ndani mwake kuna maelfu ya askari askari wa serikali wa FARDC, mgambo FADLR, polisi wa serikali waliosalimu amri kwa vikosi vya SADC na UN Umoja wa Mataifa kuomba hifadhi ya ulinzi, huku mazungumzo ya M23 na serikali ya Kinshasa yakishinikizwa kuanza.

Kuzingirwa kwa kambi hizo za SAMIDRC na MONUSCO bila kudhuriwa waliopo ndani yaani askari wa SADC na wale wa FARDC walioomba hifadhi, na wote kutodhuriwa kwa miezi miwili sasa ni uthibitisho wa nidhamu, malengo na weledi wa majeshi ya M23.

Teddy Mazina akihojiwa studio ya New Times Rwanda asimulia jinsi vyombo vikubwa vya habari duniani vilivyoamua kususia kufika Goma, Masisi, Rubaya na maeneo mengine ya Kivu ya Kaskazini na Kivu ya Kusini yanayokaliwa na M23...

Vyombo hivyo vya kimataifa vilisimulia kutoka mbali kuwa kuna watu zaidi ya 7,000 walikufa katika mji wa Goma kufuatia mapigano baina ya waasi wa 23 na vikosi vya serikali, SAMIDRC, MONUSCO wakati siyo kweli ni kiasi cha watu 300 wengi wao wakiwa ni askari wa FARDC, FDLR na kiasi kidogo sana M23

Hivyo vyombo vya habari vikubwa duniani kukosa kuona wanachosimulia kwa kuwa vyombo vikubwa vya habari vinategemea wawakilishi wao waliopo Nairobi, Kigali, Johannesburg kuripoti yanayotokea majimbo ya Kivu yanayokaliwa na M23...na mara nyingi vita vikubwa huambatana na vifo vingi tofauti na kilichotokea katika mji wa Goma wenye wakaazi milioni mbili.

Mbinu za kijeshi za M23 zinapaswa kusomwa na makamanda wa kijeshi katika meza za kupanga mapigano ya kijeshi jinsi M23 ilivyoweza kukabiliana na majeshi mengi ya kiserikali, kikanda na kimataifa huku upotevu wa maisha ukiwa mdogo tofauti na mazoea pia historia ya kivita Afrika anasema Teddy Mazina ..

Mfano mwingine eneo la Rubaya Nord Kivu (Kivu ya Kaskazini) ambapo kampuni ya madini ya Afrika ya Kusini walimegewa pande kubwa na watawala wa Kinshasa Mzee Laurent Kabila, pia siku za karibuni Felix Tshisekedi kuna migodi ya wazi ya wachimbaji wadogo kwa maelfu, ambayo yalikuwa maeneo serikali ya Kinshasa inategemea mapato mengi lakini sasa yanakaliwa na waasi wa M23 wenye nidhamu. Askari wa M23 hawaruhusiwi kuonekana wakiwa katika uniform wala kubeba bunduki.

Hivyo kutokana na nidhamu hiyo wachimbaji wadogo wanaendelea na kazi zao kwa usalama bila hofu tofauti na wakati majeshi ya serikali ya FARDC na mgambo mamluki walipokuwa wameyakalia walikuwa wamezaga huku wamevaa uniform na silaha pia kuwapora mali na madini wachimbajibhao wadogo mwandishi Teddy Mazina anasimulia.

Teddy Mazina, Burundian photo-journalist, is a political exile living between Belgium and Rwanda and a self-described “ ...
 
SADC sio wajinga lakini Tshisekedi ndiye mjinga na kwa jinsi hii Kongo wataendelea kuwa maskini mpaka watakapopata akili
 
Wameamua kuachana nae kwasababu ni mpuuzi
Binafsi naona huu ni mtego Kwa Rwanda. Sitaki kufafanua hapa. Something fishy and big is cooking. Tusubiri Muda utaongea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…