Viongozi wa Simba SC mnaonisoma GENTAMYCINE 24/7 hapa tafadhali nifikishieni hili Tamko langu Takatifu na Tukuka kwa Wachezaji wote wa Simba SC

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
TAMKO TAKATIFU NA TUKUKA

Waambieni hakuna Mchezaji mkubwa kuliko Simba SC yetu, Wameikuta na Wataiacha / Watatuachia. Huu Mtindo wa Kucheza Mpira kwa Kudekadeka, Kuringa na kama Wanalazimishwa uwe mwanzo na mwisho. Kama kuna Mchezaji anaona Simba SC siyo mahala pake aombe avunjiwe Mkataba wake upesi sana na atupishe.

Kuanzia Mchezo weru wa Ligi Kuu ya NBC ya Jumatano au Alhamisi dhidi ya Coastal Union FC Uhuru Stadium ( Shamba la Bibi ) Saa 10 Kamili Jioni tunataka kuona mabadiliko makubwa kwa Wachezaji kujitoa kweli huku wakivuja Jasho na ikiwezekana watokwe hata na Damu kwa ajili ya Kuipambania Simba SC yetu.

Wasipobadilika na wakiendelea na huu Upuuzi wao kiukweli Watatusamehe kwani wale ambao tunawamudu Kiubavu tutawapiga mno tu Viwanjani na hata Mitaani / Maskani tunakokaa na kukutana nao Kutwa na kwa wale ambao kutokana na Kukomaa Kwao na kuwa na Nguvu nyingi na Ubavu hatutoweza Kuwapiga tutakachofanya ni Kuwapopoa tu kwa Mawe au hata Kuvunja Vioo vya Magari yao ya Kifahari.

Tumechoka kwakweli.

Wenu Mtoa Tamko Mkuu GENTAMYCINE.
 
Simba timu nzuri ila mashabiki tunapenda mpira wa kitoto pasi nyingi tobo kanzu visigino "objective football" pasi tatu tupo golini wanaona timu bado ila ipo siku wataelewa,,,,timu kama Al ahly au Wydad uchezaj wao kwenye knock out stage ukiziangalia hata hazifutii na uwezi amini ndio znashinda mataji na miaka miwili zmecheza final,

Ukiwacheki mamelody wanavyotakata na pasi pasi zao unaweza ukasema miaka yote wao ndio wanaochikua ubingwa wa Africa,kumbe mara ya mwisho ubingwa walichukua 2016,leo Wydad casablanca katoa sare 1-1 na Hafia ya Guinea,na mtaona kesho kutwa Al ahly na st george akiwa ugenini matokeo yatakavyokua na watakavyocheza halafu mje muangalie mechi za marudiano hizi timu kubwa zitakavyopita kwa matokeo ya jumla,

Timu kubwa zinatakiwa zicheze kikubwa sio kototo kushangilia visigino,Simba hii itakuja kuwa hatari sana kuliko ile iliyotolewa na Wydad kwa penalties kule Morocco mkitaka kuamini mtaona kwenye mechi kubwa tutakavyocheza msimu huu,kumbukeni haya maneno.
 
Kwenda huko michezaji haijitumi kazi kucheza kimamamama.
 
Clatous Chota Chama.
Chama wa Robertinho kabadilika sana anaanzia ku press kule kule juu,anakimbia hadi klabu bingwa tunatolewa msimu uliopita waliongoza kwa faulo ni Saidoo, Chama, Baleke na Kibu,,ile mechi ya juzi Chama alivyokus anacheza nyuma ya Phiri Kipindi cha kwanza kweli hakuonekana ila kipindi cha pili alivyokua anacheza nafasi anayoipenda kuwa free kutokea wide pembeni kushoto tumeona hatari yake,namba za Chama ni kubwa kwenye ku defend kuliko hata Kanoute.
 
Timu mbovu hasa kanoute, mzamiru na beki za pembeni hamna kitu
Kama ni shabiki mwenzangubwa simba nasikitika ya kuwa na shabiki wa simba mwenye akili za kiutopolo mzamiru injini ile halafu siku zote "class is permanent but form is temporary" konachotekea sasa no form tuu class ya kapombe,Tshabalala inajulikana inaitajika mda na nafasi hawa wote watarudi katika ubora wao, kanoute naungana nawewe labda kwakua kanoute mpira wake ni wakufundishwa sana darasani hana uwezo binafsi ni mchezaji wa mbinu na mipango ya mwalimu sana,kwa uchezaji wake apambane sana maana namba atapoteza maana kuna mda unatakiwa uonyeshe uwezo binafsi kanoute kitu icho hana

Sent from my SM-G9650 using JamiiForums mobile app
 
Bado hamjasemaa,mtasema tuu

Sent using Jamii Forums mobile app
Simba msimtafute mchawi mlijibweteka sana mlipopata ngao ya jamii. Yanga ilipoliachia kombe la jamiii ilitasmini timu nzima na kuwapigia makelele mafoward wake kuwa ni butu. LEO simba kutoka sare pale zambia tuu basi wanalaumu wachezaji! mbona sare ya finali ya ngao ya jamii hamkumlaumu mchezaji ?

Kumbukeni ya kuwa Power dynamoo ya zambia sio timu ndogo na isingekubali kufa kikike nyumbani kwao/. Tafadhali sana SSC kaa chini utasmini makosa ili usonge mbele. Kocha wenu ni mzuri sana ila bahati ya ushindi haiukuwa yenu.
 
Timu mbovu hasa kanoute, mzamiru na beki za pembeni hamna kitu
hakuna mchezaji wa kulaumiwa kwa sababu tangia mshinde ngao ya jamii mlikuwa na kiwewe cha furaha mpaka jana jioni. iweje haya yote ya kulaumu wachezaji yaje leo wakati wa ngao ya jamii mliwasifia?mkiisha ikamia yanga tuu basi hamuoni makosa ya wachezaji ila mkishindwa tuu basi mnaanza kuwapeleka keko wachezaji wenye makosa uwanjani. huu ni umafamba.
 
Mashindano haya ya kimataifa kama simba imefanikiwa kutoka sare ugenini basi ipongezeni timu yenu. zamareki jana kadhalilishwa mbili nunge pale djibout naleo iweje simba badala ya kushangilia sare inajiona ilikuwa na hadhai ya kushinda. mashindani ya mabingwa wa CAF isibezwe timu yeyote.

Kila timu ina kocha mjanja ambaye kusuka ushindi uwanjani kama simba iliambulia sare basi iongeze mbinu badala ya kuanza kulaumu wachezaji. hawa power dynamoo sio wa kuwachezea. Power dynamoo kila mwaka hutolewa kwa mbinde sana mashindanoni hivyo kama wamejiuliza na kusawazisha mashimo yao usitegemee hata Al Ahly ya misri ingefua dafu pale Northen Rhodesia jana.
 
Hii game ya wadjibout na zamalek si imepigwa hapa bongo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…