Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
Wala sio hesabu ngumu. Ni wazi sana kwamba taasisi kama Polisi na NEC mara kwa mara zinafanya ukosefu mkubwa wa usawa dhidi ya vyama vya upinzani. Umewahi kujiuliza kwa nini?
Sababu ni moja, viongozi wa taasisi hizi wanajua wazi kwamba Upinzani ukichukua serikali wataondolewa madarakani kutokana na ukiukwaji wa taratibu za kikazi wanaoufanya mara kwa mara. Na baadhi yao wanajua kwamba huenda hata wakafunguliwa mashitaka na kufungwa kwa mambo waliyofanya.
Hata mimi ningekuwa Lissu, nikishinda Urais watu wa kwanza kuondoka ni kama IGP kwa kusimamia Polisi inayokiuka maadili ya kazi, Mkurugenzi wa NEC kwa upendeleo wa wazi, Mwendesha Mashitaka wa serikali, Mwanasheria Mkuu wa serikali, watu wanaosimamia vyombo vya habari nk. Hawa watu ningewatoa bila kuchelewa kwa sababu utendaji wao wa kazi umekuwa wa kisiasa badala ya kitaaluma, sio suala la kisasi.
Kwa mfano, unafikiri Polisi walishindwa kupeleleza na kuwatia hatiani watu wa kikundi cha Wasijulikana? Unafikiri hawakijui? Sasa jiulize, ikiwa Tundu Lissu anashika madaraka, jambo moja wapo kuu atataka lichunguzwe kwa kina ili waliohusika wachukuliwe hatua halitatia ndani wasiojulikana? Unafikiri baadhi ya maofisa wa polisi na hata TISS watapona katika hilo?
Kwa hiyo basi, kupona kwa viongozi wa polisi na taasisi kama NEC wasifukuzwe kazi na hata kufunguliwa mashitaka ni wao kufanya kila wawezalo ili CCM ishinde tena. Hapa sio suala la kuipendelea CCM wanalofanya, ni suala la survival yao wenyewe. Hawa watu wanajua wazi kwamba kuwatendea haki watu wa upinzani ni sawa na wao wenyewe kujiweka kamba ya kujinyongea shingoni. Hawafanyi ukiukwaji mkubwa wa haki dhidi ya wapinzani kwa ajili ya CCM bali ni kwa ajili yao wenyewe.
Wapo makamanda wa polisi wengi waliowanyanyasa wapinzani kwa hulka yao wenyewe au amri toka juu, na wanajua wazi kwamba kwa mfano, Tundu Lissu akishinda basi huo ndio utakuwa mwisho wa vibarua vyao. Kwa jinsi hiyo watafanya kila wawezalo kutaka kumkwamisha Tundu Lissu asishinde.
Huo ndio ukweli wa mambo.