Uchaguzi 2020 Viongozi wa taasisi kama Polisi na NEC kuibeba CCM dhidi ya vyama vya upinzani ni kuelewa kwamba wapinzani wakichukua serikali wataondolewa vyeo vyao

Uchaguzi 2020 Viongozi wa taasisi kama Polisi na NEC kuibeba CCM dhidi ya vyama vya upinzani ni kuelewa kwamba wapinzani wakichukua serikali wataondolewa vyeo vyao

Synthesizer

Platinum Member
Joined
Feb 15, 2010
Posts
12,699
Reaction score
22,598
Wala sio hesabu ngumu. Ni wazi sana kwamba taasisi kama Polisi na NEC mara kwa mara zinafanya ukosefu mkubwa wa usawa dhidi ya vyama vya upinzani. Umewahi kujiuliza kwa nini?

Sababu ni moja, viongozi wa taasisi hizi wanajua wazi kwamba Upinzani ukichukua serikali wataondolewa madarakani kutokana na ukiukwaji wa taratibu za kikazi wanaoufanya mara kwa mara. Na baadhi yao wanajua kwamba huenda hata wakafunguliwa mashitaka na kufungwa kwa mambo waliyofanya.

Hata mimi ningekuwa Lissu, nikishinda Urais watu wa kwanza kuondoka ni kama IGP kwa kusimamia Polisi inayokiuka maadili ya kazi, Mkurugenzi wa NEC kwa upendeleo wa wazi, Mwendesha Mashitaka wa serikali, Mwanasheria Mkuu wa serikali, watu wanaosimamia vyombo vya habari nk. Hawa watu ningewatoa bila kuchelewa kwa sababu utendaji wao wa kazi umekuwa wa kisiasa badala ya kitaaluma, sio suala la kisasi.

Kwa mfano, unafikiri Polisi walishindwa kupeleleza na kuwatia hatiani watu wa kikundi cha Wasijulikana? Unafikiri hawakijui? Sasa jiulize, ikiwa Tundu Lissu anashika madaraka, jambo moja wapo kuu atataka lichunguzwe kwa kina ili waliohusika wachukuliwe hatua halitatia ndani wasiojulikana? Unafikiri baadhi ya maofisa wa polisi na hata TISS watapona katika hilo?

Kwa hiyo basi, kupona kwa viongozi wa polisi na taasisi kama NEC wasifukuzwe kazi na hata kufunguliwa mashitaka ni wao kufanya kila wawezalo ili CCM ishinde tena. Hapa sio suala la kuipendelea CCM wanalofanya, ni suala la survival yao wenyewe. Hawa watu wanajua wazi kwamba kuwatendea haki watu wa upinzani ni sawa na wao wenyewe kujiweka kamba ya kujinyongea shingoni. Hawafanyi ukiukwaji mkubwa wa haki dhidi ya wapinzani kwa ajili ya CCM bali ni kwa ajili yao wenyewe.

Wapo makamanda wa polisi wengi waliowanyanyasa wapinzani kwa hulka yao wenyewe au amri toka juu, na wanajua wazi kwamba kwa mfano, Tundu Lissu akishinda basi huo ndio utakuwa mwisho wa vibarua vyao. Kwa jinsi hiyo watafanya kila wawezalo kutaka kumkwamisha Tundu Lissu asishinde.

Huo ndio ukweli wa mambo.
 
Magufuli kwenye Kampeni Arusha Tarehe 23 October...atapokelewa na Mabango ya FAO LA KUJITOA

Wengi Arusha walipoteza Kazi na Kukosa Haki ya kulipwa pesa zao.

Arusha watu wengi mno walipoteza Kazi kutokana na Korona, utalii uliathirika

NSSF waligoma kulipa watu pesa zao zote..
 
Suluhisho litakalofanyika na hii jamii uliyoitaja ni kutompigia kura huyo T.Lissu ili walinde pension zao.
 
Msikilkilize Mzee Butiku hapa kwenye hii video clip. View attachment 1601932
Kwani yeye ndo haogopi? Huwa wako wapi kukemea lolote wanaloona haliko sawa? Manake wao Wana nafasi na hasa huyu Butiku maana yeye anatoka taasisi inayohusiana na kuleta amani , maendeleo na maelewano ya mwl Nyerere.

Ajabu huoni neutrality ya hiyo taasisi, ni kama CCM nyingine tu. Hawa wazee wakiwa hata na Jambo wanaloona haliko sawa na wanataka kuliongea, huwaoni wakiongea wazi na lugha rahisi. Wakati wote utawaona wanaongea mafumbo, na kuzunguka kwingi kana kwamba hilo wanaloliongea hawaliamini. Je huo siyo uoga?

Wengine ndo kabisa siku hizi wako huko na wanatetea Mambo ambayo dhairi shairi hawayaamini. Kuna pole pole, kabudi na hata jaji warioba. Sitasahau jaji warioba alivyopuuzwa na WABUNGE wa CCM wakati wa bunge la katiba. Ajabu uchaguzi uliofuata ndo alikuwa jukwaani kunadi Mambo ambayo hata yeye hayaamini. Je huo siyo uoga? Kama siyo jasiri kusema bora unyamaze, badala ya kuwa double minded.

Unajua sio tu viongozi ndo huichonga jamii, aina ya watu wanaoongozwa pia huwachonga viongozi. Kama kutatokea viongozi wetu kwa namna yoyote kufanya vibaya, uzembe, kutojali, udikteta, rushwa nk. Ni kwa sababu waongozwa nao hawawachongi viongozi( they don't shape their leaders) kwa kuwaambia makosa yao nk.

Na hasa wananchi waliopata fursa( platform) akiwemo Butiku pia. I am eagerly longing to see the kind of wananchi who are in the position of shaping their leaders. May we get rid of the mentality where,we only depend on leaders to shape the community. We both depend on each other, as shaping is all concerned.

Wasalaam.
 
... that's the fact! Unategemea Lissu aingie madarakani Sirro aendelee kuwa IGP? Au Mahera aendelee kuwa Mtendaji Mkuu wa NEC? Au Mutungi aendelee kuwa Msajili wa Vyama vya Siasa? Hicho kitu hakipo!

Na hapo ndipo unapokuja umuhimu wa Rais kupunguziwa madaraka kikatiba; zaidi ya 80% ya teuzi za watendaji wa juu anafanya yeye wakati tenure yake ni just 5 yrs.

Wenye akili zao wanapendekeza nafasi hizi badala ya kuwa za "fadhila" watu waingie kwa sifa zao; hata aje nani, uko pale kwa competence utaendelea kuwepo tu no matter who is in power! Akili ndogo hili hawalioni badala yake kila uchaguzi ni kuliweka taifa kwenye tension kulinda madaraka yao!
 
Na hao ndio mara zote hujipa jina la wazalendo, ila sihivyo wanatetea matumbo yao tu. Kwa namna ilivyofeli awamu hii hakukua na haja ya upinzani kufanya kampeni au ingebidi ushindani uwe kati ya Lissu na Lipumba na si Magufuli.
 
Kumbe Mgufuli ndo aliileta eeeh?

Nhiiiiiiiiiiiiii, ngoja nicheke tu 😂😂😂😂
Hivi mnalishwaga nini huko Lumumba?

Point hapo Ni FAO la kujitoa...Hiyo Ni akiba ya Mfanyakazi....NSSF walipe wanyonge akiba zao Zote.

Huo sio mikopo, Ni Haki, Ni akiba za watu.

Kikwete alilipa, MKAPA alilipa...why Magufuli aondoe FAO la kujitoa?
 
Hivi mnalishwaga nini huko Lumumba?

Point hapo Ni FAO la kujitoa...Hiyo Ni akiba ya Mfanyakazi....NSSF walipe wanyonge akiba zao Zote.

Huo sio mikopo, Ni Haki, Ni akiba za watu.

Kikwete alilipa, MKAPA alilipa...why Magufuli aondoe FAO la kujitoa?
Mimi sijazungumzia kuhusu FAO la kuijtoa,angalia nimemquote nini sio kukurupuka tu.
 
Kumbe Mgufuli ndo aliileta eeeh?

Nhiiiiiiiiiiiiii, ngoja nicheke tu [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Mkuu so hapo umeelewa kuwa Jiwe ndiye alileta corona? Jamani fisiemu huwa wanawatoa wapi watu kama wewe?
 
Mkuu so hapo umeelewa kuwa Jiwe ndiye alileta corona? Jamani fisiemu huwa wanawatoa wapi watu kama wewe?

Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
Eti hao ndio watetezi wa CCM , duh. Kazi ya kutetea uovu Ni ngumu mnooo.

Huyo jamaa hajaelewa point Ni FAO la kujitoa

Nssf wamefilisika, Pesa za watu wamepeleka wapi?
 
Kumbe Mgufuli ndo aliileta eeeh?

Nhiiiiiiiiiiiiii, ngoja nicheke tu 😂😂😂😂
Hujaelewa. Kwa sababu ya Korona, watu wengi wamepoteza kazi. Magufuli hajaleta korona. Lakini fao la kujitoa lingekuwepo, hao waathirika wangepata kifuta machozi katika kipindi hiki kigumu. Hapo ndio makosa ya Magufuli
 
Kwa kuzingatia sheria na haki zao zitazingatiwa kikamilifu bila uonevu wowote,hivyo wasiwe na shaka wala hofu.Watatikiwa kutoa ushahidi kamili na kila mmoja atendewe anavyostahili.
Hawa adhabu yao siyo kuondolewa pekee ni kushitakiwa kwa matumizi mabaya ya ofisi za umma.
 
Kwenye hili upo sahihi, though changamoto kubwa ni uelewa tu. Hata Rais awe Lissu, Lipumba au Sipunda kama umeajiriwa Serikalini na una mkataba wa kudumu hutakiwi kuwa na hofu ya kupoteza cheo provided kuwa una taaluma yako iliyokupa hiko cheo.

Wito kwa watumishi wa Umma( NEC/Polisi n.k) ni kutenda haki. Hakuna mtu atachukua mshahara wako kwa Lissu kushinda, sanasana mtaongezwa mishahara kama alivyohaidi kwenye kampeni zake pamoja na areas ukizingatia tangu 2015 hadi 2020 hakuna nyongeza ya mshahara iliyotolewa kwa mtumishi wa Umma
 
... that's the fact! Unategemea Lissu aingie madarakani Sirro aendelee kuwa IGP? Au Mahera aendelee kuwa Mtendaji Mkuu wa NEC? Au Mutungi aendelee kuwa Msajili wa Vyama vya Siasa? Hicho kitu hakipo!

Na hapo ndipo unapokuja umuhimu wa Rais kupunguziwa madaraka kikatiba; zaidi ya 80% ya teuzi za watendaji wa juu anafanya yeye wakati tenure yake ni just 5 yrs. Wenye akili zao wanapendekeza nafasi hizi badala ya kuwa za "fadhila" watu waingie kwa sifa zao; hata aje nani, uko pale kwa competence utaendelea kuwepo tu no matter who is in power! Akili ndogo hili hawalioni badala yake kila uchaguzi ni kuliweka taifa kwenye tension kulinda madaraka yao!
Hilo ni kweli na wazalendo wa nchi hii wanalipigania hasa kupitia Katiba mpya ya Wananchi.Tuchague mabadiliko kupitia sera za Uhuru,Haki na Maendeleo ya wote.
 
... that's the fact! Unategemea Lissu aingie madarakani Sirro aendelee kuwa IGP? Au Mahera aendelee kuwa Mtendaji Mkuu wa NEC? Au Mutungi aendelee kuwa Msajili wa Vyama vya Siasa? Hicho kitu hakipo!...
Well said Mkuu! Huo ndio ukweli
 
Back
Top Bottom