Viongozi wa Tanzania(wengi) hawajawahi kuomba kazi katika maisha yao

Viongozi wa Tanzania(wengi) hawajawahi kuomba kazi katika maisha yao

Kijakazi

Platinum Member
Joined
Jun 26, 2007
Posts
10,860
Reaction score
18,819
Kama ulishawahi kutafuta kazi na kupata kwa maana ya kutuma maombi kwanza kujipima hata kama unastahili tu kutuma maombi, kuwa short listed kuitwa Interview ya kwanza na ya pili na mwishowe kushinda na kupata kazi, basi utaelewa ni jinsi gani ilivyo ngumu kupata kazi na nini ufanye ili usiipoteze na hata ukiona mtu hana kazi au anatafuta kazi utaelewa na kumhurumia.

Lkn Viongozi wetu wengi hasa wazee hawajawahi kuomba kazi katika maisha yao, wengi wao walifanyiwa kila kitu wakati wa Ujamaa, wengine hata walifwatwa na kupewa kazi bado wakiwa Sekondari jaribu kuongea na Mzee unayemfahamu aliye serikalini jinsi alivyopata kazi.

Wengine wamepitia CCM kama chipukizi mpaka juu, hakuna popote alipotuma maombi ya kazi, kuhakikiwa na kuna short listed, hii inaelezea labda kwa nini wako sooo out of touch na reality na kuongea ujinga na kuonekana kama wanakebehi wasio na kazi …
 
Back
Top Bottom