Viongozi wa TFF na Bodi ya Ligi Wanahujumu Chama na Serikali Kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Mwaka Huu 2025

Kitimoto

JF-Expert Member
Joined
Aug 25, 2012
Posts
8,198
Reaction score
9,911
Wanachokifanya Chama cha soka nchini TFF na Bodi ya Ligi kuhusiana na mechi ya mkondo wa pili ya watani wa jadi Young Africans SC na Simba SC ni wazi wanatumika na baadhi ya wanasiasa kuhujumu uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Ikumbukwe vilabu hivi vikubwa vina wanachama na mashabiki ambao wale wenye sifa za kupiga kura sehemu kubwa wapo kwenye vilabu hivi.

Maneno ya Waziri husika aliyoyaongea Bungemi inaonesha kama vile si miongoni mwa mwanaCCM anayeitakia mema awamu iliyopo madarakani, aliyoyaongea yamezidi kuleta maswali mengi kutoka upande mmoja wa hivi vilabu kwa kujiona wanaonewa ikizingatiwa tunaelekea kwenye Uchaguzi Mkuu.

Nashauri kwa uongozi wa nchi ili jambo fanyieni kazi kwa haraka mtakuja kunishukuru baadae.
 
CCM wala haihitaji kura za wanayanga kushinda uchaguzi hivyo ni vitisho vya kitoto sana!

Inashindwa na nani hii 2025? Rungwe au Dovutwa?
 
Naendelea kusisitiza kwamba Viongozi wa TFF ni kikundi cha wahuni waliojificha kwenye uongozi wa soka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…