VIongozi wa Ulaya waenda Kyiv kwa gari moshi kuiomba Urusi isitishe Vita na Ukraine

VIongozi wa Ulaya waenda Kyiv kwa gari moshi kuiomba Urusi isitishe Vita na Ukraine

Webabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2010
Posts
10,509
Reaction score
16,734
Vita vya miaka mitatu vimetoa funzo kubwa kwa mataifa makubwa duniani pamoja na Ulaya.

Wakiwakilisha wenzao,viongozi watano wa mataifa ya Ulaya walifika mjini Kyiv hapo juzi na kukushanyika kwa pamoja na raisi Zelenky kwa madhumuni ya kuitaka Urusi iongeze muda wa usitishwaji vita kutoka siku 3 mpaka 30.

Kutokana na mazingira ya vita viongozi hao walilazimika kutumia garimoshi ya pamoja na kuiarifu Urusi kuhusiana na ugeni wao nchini Ukraine.

Baada ya kutembelea maeneo mbali mbali ya mji huo viongozi hao kwa pamoja walikaa kwenye meza kuizunguka simu na kumpigia mwenzao raisi Trump wa Marekani ili kutaka uungaji mkono wake kwa maombi yao kwa raisi Vladmir Putin juu ya haja ya kusitisha vita.

Pamoja na kwamba wao ndio waliotaka usitishwaji vita huo,viongozi hao bado walijaribu kujikweza na kumtishia raisi Putin kwamba asipokubali kuisitisha vita basi wao watamuongezea vikwazo vya kiuchumi.

Majibu ya Urusi kwa salamu hizo za viongozi wa Ulaya ilikuwa ni kupiga kwa nguvu kwa kutumia droni maeneo kadhaa ya Ukraine mbali na Kyiv.

Nchi za Ulaya zote kwa sasa zimeathirika sana kiuchumi kutokana na vita vya Ukraine na Urusi.Mataifa hayo ya Ulaya kikawaida huwa yanaishi kiujanja ujanja kwa kuzinyonya nchi maskini hasa za Afrika kwani nchi hizo hazina raisilmali za kutosha na mazao ya kilimo.

Katika hali ya usalama mataifa hayo pia huwa yanapata bidhaa nafuu za nafaka na nishati kutoka Urusi na Ukraine.Hivyo uamuzi wao wa kuongeza kasi ya usitishwaji vita ni katika kutambua athari iliyoletwa na vita hivyo kwao.
 
Wameenda kwa sababu za kimaslahi wanaona marekani amesaini mkataba wa kuijenga Ukraine na amepata faida

kwanini hawakwenda kabla?

Vita ilishaisha
 
Wameenda kwa sababu za kimaslahi wanaona marekani amesaini mkataba wa kuijenga Ukraine na amepata faida

kwanini hawakwenda kabla?

Vita ilishaisha
Washike akili zao.
Baada ya vita hivi dunia itakaa miaka 50 bila kuchokozana.
 
Back
Top Bottom