MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 21,387
- 44,030
Habari wakuu.
Baada ya kupokea meseji zenu zisizo na idadi na pia simu nyingi za kunisihi niseme neno kuhusu hii hali iliyojitokeza ya viongozi wa upinzani kuondoka nchini kwa madai ya kuepuka hatari zinazowakabili dhidi ya maisha yao.
Ninachoweza kwa ufupi ni kwamba nimesikitishwa na hizo taarifa na wanaoweza kutoa majibu na kuchukua hatua ni vyombo vya usalama. Ninaamini wanausalama wako kazini.
Lakini baada ya kutafakari kwa kutumia akili nyingi sana ambazo wafuasi wengi wa upinzani hawana nikagundua kitu. MADENI. Ndiyo ni MADENI.
Naona hili ni jambo ambalo halitajwi sana lakini linachochea baadhi ya viongozi wa upinzani hasa waliokosa ubunge kuona namna nzuri ya kukimbia madeni ni kufanya wanachofanya sasa.
Mh Ndugai alishadokeza uma kuhusu hili jambo na kumtaja Mh Lema kama mmojawapo wa wanaodaiwa madeni makubwa. Ninawasihi viongozi wengine wa upinzani wanaotarajia kuikimbia nchi wajitahidi kulipa madeni kwanza au wawaelekeze wanaowadai namna ya kupata pesa zao wakati watakapoondoka.
Nawasilisha