Mtanzanias
JF-Expert Member
- Jul 30, 2021
- 1,747
- 3,725
Nimeifuatilia hii timu ya wanawake kwa mda mrefu lakini naona viongozi ni Kama vile wameitelekeza, awaweki nguvu kuakikisha hii timu inakuwa stable kiushindani, aiwezekani timu inakuwa inafungwa tu kiholela na simba kila wanapokutana karibia msimu wa 4 sasa akuna mbinu mbadala ya kujinasua na kuleta ushindani, leo Hii kocha Edna lema anahojiwa anaongea pumba eti ingekuwa inafundishwa na mwanaume ingeshinda!!! Kwaiyo mwanaume ndo angeingia uwanjani kufunga magoli au kitu gani? Anashindwa kuongea ukweli timu inatakiwa ifanye usajili wa maana kwa wachezaji wenye uwezo wa kuichezea yanga na sio kuokota wachezaji ilimradi kujaza nafasi, kocha lema ni mzuri lakini inaonekana apewi ushirikiano wa kutosha kuitengeneza timu ya kiushindani na yeye anabaki kusononeka moyoni, simba wao timu yao waliitengeneza mda mrefu wakaweka nguvu na sapoti kubwa kwenye ile timu ndo maana wanafanya vizuri lakini yanga princes ilitelekezwa na haipewi kipaumbele ni bora ivunjwe tujue moja, kwa hili viongozi mmetuangusha Sana tena sana, fanyeni jambo kwenye timu ya awa dada zetu tuepuke hii aibu ya kuwa wateja kwa simba kila tunapokutana