Kumekuwa na udhalilishaji mkubwa juu ya brand ya Yanga kwa kisingizio cha utani wa jadi kinachofanywa na Kiongozi wa Simba anayejiita Hajji Manara.
Nimefuatilia kwa karibu ndani ya msimu huu mtu huyo amefanikiwa kuharibu biashara nyingi za Yanga.
Pengine angekua tu mshabiki tungejua namna ya kudili nae sisi mashabiki lakini sababu ni kiongozi ndani ya Simba basi Yanga inapaswa kudili nae kwa sheria na kanuni za mpira.
Mtu huyu amefanikiwa pakubwa kuharibu biashara ya Madela ya Yanga, Kalenda za Yanga na jezi za Yanga hivi karibuni. Si ajabu akaitwa kwenye kipindi cha redio na kutumia masaa yote matatu kukandia bidhaa za Yanga na kuisemea Yanga kuliko klabu yake inayomlipa mshahara. Hii haikubaliki na sio swala la kuleta utani wa jadi kwenye biashara.
Kama haitoshi amekua akifanya personal attack kwa Mwenyekiti msaidizi wa Yanga ndugu Mwakalabela juu ya maumbile yake kwa maneno na picha za kudhihaki.
Mwanzoni nilidhani ni watani personal lakini kwenye press ya leo ya Mwakalebela kaonyeshesha hawana utani wowote wa kibinafsi. Kutokana na viongozi wa Yanga kusema wamechukua hatua zote kumshtaki TFF lakini shirikisho limekua kimya kuchukua hatua nashauri yafutayo yafanyike :
Kumtangaza Manara kama adui namba moja wa Yanga alieshindikana hata na TFF. Hii iende sambamba na kuachana na kampuni zote zilizompa ubalozi mtu huyo kwani ndizo zinazompa kibuli cha kuharibu brand za kampuni nyingine.
Kutafuta watu wa kudili nae nje ya sheria za TFF hasa mitandaoni mana ni wazi wameshindwa kumrekebisha mtu huyo kufuata sheria ambaye wakati mwingine anaonekana ni Chanzo kikubwa cha uhasimu baina ya mashabiki.
Kuishtaki TFF kwa baraza la michezo BMT juu ya uonevu mkubwa wa kushindwa kuchukua hatua juu ya kesi zinazowasilishwa na Yanga.