Hii kitu nimeipenda sana, viongozi wa yanga wamepata shutuma za Kila aina wiki hizi tatu, timu ya yanga imechambuliwa na Kila mchambuzi na maneno yake, kocha kafukuzwa na wachambuzi.
Lawama za Kila aina zimerushwa kwa yanga baada ya kupoteza mechi 2 dhidi ya Azam na Tabora united, lakini hakuna kiongozi yoyote wa Yanga aliyetoka kauli yoyote juu ya hayo yote!
Wamekaa kimya wakiendelea kuyafanyia kazi yale yote yanayotakiwa kufanyiwa kazi,
Wanafanya mipango yao kiuweledi na sio kupayukapayuka ovyo.
Tunajua Kuna wachambuzi wako kwenye payroll ya klabu Fulani wanajaribu kuchokonoa kujua kinachoendelea ili waupate cha kuandika kwenye mitandao yao lakini wamepigwa Pini hawajui chochote wamebaki kuwa watabiri kama waganga wa kienyeji, Leo wanapost hiki kesho wanaposti kile awaeleweki!
Viongozi wameamua kunyamaza kufanya tathmini ya kina kujua ni wapi waliteleza na ni wapi warekebishe baada ya hapo Kuna kitu kinatengenezwa na watu watafunga Tena midomo waanze habari za gsm anaharibu ligi!
Wakati huu wako kimya wanakenua na meno yote 32 yanaonekana lakini wakianza kupoteana utaanza kusikia zile KELELE zinaibuka Tena za gsm anaharibu ligi!
Viongozi chapeni kazi nafikiri mmeona wanafiki wengi kipindi hiki, wanataka mpoteane wafurahie kwa maana iyo akuna habari za GSM anaharibu ligi bali ni wivu unawasumbua mkirudi kuanza ligi msicheke na kima iwe ni mwendo wa kata funua mpaka mwisho!