Lusungo
JF-Expert Member
- Jan 4, 2014
- 29,524
- 42,677
Nimeisikiliza hotuba ya Rais Mwinyi imenishangaza sana.
Nimejiuliza na kutafakari sana kuwa kama viongozi hawa waliopewa kila aina ya nyenzo ili ziwawezeshe kufanya kazi wanalalama je, wananchi wa kawaida wafanye nini? Wapeleke wapi kero na malalamiko yao? Kama Rais anaweza kuuona ufisadi wa kutisha kwa miaka miwili anaagiza vyombo vifanye kazi na vinakaa kimya nini hatima ya nchi?
Naliona neno "mkalitizame/mkajitathmini/mkajipange/mkajiratibu/mkajifikirie" kuwa kichaka cha watawala wetu kukwepa majukumu. Nimeliona hili kwa Rais Samia na sasa naliona kwa Rais Mwinyi! Huu ufisadi unaotamalaki nani atauondoa ikiwa wenye jukumu hilo mnaawambia wakalitizame? Wasipolitizama au kujitathmini nani atafanya?
Kuna ombwe kubwa la uongozi hapa nchini na soon tutashuhudia mazito zaidi ya Tegeta Escrow!
Jionee video hapa chini.